Madereva wa bodaboda sasa ndani ya tochi

Mtanzania - - Kanda - Na RAYMOND MINJA

TABIA ya waendesha pikipiki (bodaboda), wanaowavunja miguu askari wa usalama barabarani kisha kukimbia sasa imepatiwa dawa baada ya jeshi hilo kuja na kamera maalumu ya kupiga picha namba za magari na pikipiki zinazofanya makosa.

Kumekuwa na desturi ya madereva wa magari na pikipiki kuwagonga kwa makusudi askari wa usalama barabarani, lakini hawatiwi mbaroni.

Akizungumza wakati wa ufungaji mafunzo ya waendesha bodaboda 180 juzi, Kaimu Kamanda wa Trafiki Mkoa wa Iringa (RTO), Inspekta Joseph Mgeri, kumekuwa na tabia ya madereva bodaboda kusababisha ajali na kukimbia ili kupunguza ongezeko la ajali za barabarani.

“Shida kubwa ya hawa madereva wa bodaboda ni kutokuwa na elimu ya usalama barabarani na ndio maana walikuwa wakiwaona askari ni adui kwao, wakati mwingine kuwagonga na ndio maana tunatoa mafunzo haya na wale waliokuwa wakiwagonga askari na kukimbia sasa dawa inakuja tutakuwa na kamera maalumu ya kupiga picha ili mtu akisababisha ajali na kukimbia basi chombo chake kinapigwa picha na baadaye kukamatwa.

Alisema watakuwa wakitoa leseni kwa madereva waliopata mafunzo ya usalama barabarani tu na yeyote ambaye hatakuwa na cheti cha mafunzo ya usalama barabarani hataweza kupatiwa leseni.

Mratibu wa mafunzo ya elimu ya usalama barabarani mkoani Iringa, Frenk Boma, alisema mafunzo hayo yatasaidia kupunguza ajali za barabarani, kujenga mahusiano kati ya polisi na madereva pamoja na kupata leseni iliyo halali.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.