Bilioni 26/kugawiwa wanahisa wa Vodacom

Mtanzania - - Biashara - Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

ZAIDI ya wanahisa 1500 wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC, walikutana kwa mara ya kwanza mwishoni mwa wiki na kufanya mkutano na uongozi wa kampuni hiyo na kuchagua viongozi mbalimbali na kufikia mwafaka wa gawio la kwanza la hisa kwa kuwapa zaidi ya Sh bilioni 26, Novemba mwaka huu.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Tanzania PLC, Ali Mufuruki, alipokuwa akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na utoaji wa gawio hilo kwa wanahisa wake.

Mwenyekiti huyo wa bodi alisema kwamba, kila mwanahisa atapatiwa gawio hilo la shilingi 12 na senti 74.

Alisema kampuni hiyo imeamua kufanya hivyo kutokana na kuimarika vizuri kwa kujiendesha kibiashara, hivyo iliona ni vyema kutoa gawio hilo ili kila mwanahisa aweze kunufaika pale inapobidi.

Kampuni hiyo pia iliweza kufanya mkutano wake mkuu wa mwaka kwa kuwakutanisha wanachama wake kutoka mikoa mbalimbali kwa lengo la kubadilishana mawazo pamoja na kwenda sambamba na uteuzi wa wajumbe wapya watakaoingia ndani ya bodi ya wakurugenzi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Ian Ferrao, aliwapongeza wajumbe wote walioteuliwa na kuahidi kutoa ushirikiano kwa lengo la kuhakikisha hisa za vodacom zinaleta manufaa kwa wamiliki wake wote.

“Wanahisa watoe shaka kabisa kuhusiana na hisa zao, kwani zipo salama na kampuni inaendelea kufanya vizuri sokoni na ninawapongeza wajumbe walioteuliwa na ninaimani nayo, kwani itafanya kazi kwa kushirikiana vizuri na wanachama ndani nasi tutawapa ushirikiano wa kutosha ndani ya kampuni yetu,” alisema Ferrao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.