Barafu Jogging yapata viongozi wapya

Mtanzania - - Habari Za Michezo - Na GLORY MLAY

UCHAGUZI waklabu ya Barafu Jogging Sport Club , umefanyika juzi katika Hoteli ya Magomeni Dar es Salaam, huku Malic Mgala, akichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo baada ya kupata kura 47.

Mgaa aliwashinda wapinzani wake, Adamu Marinda, aliyepata kura nne kati ya kura 52 zilizopigwa na wajumbe waliohudhuria katika uchaguzi huo.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilichukuliwa na Tonny Njau, aliyepata kura 50 kutokana na hakuwa na mpinzani na kura mbili ziliharibika.

Mau Chamshama, alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, baada ya kupata kura 40, akimbwaga mpinzani wake, Kaike Siraju, aliyepata kura 12, huku msaidizi wake akipata kura 50 huku mbili zikiharibika.

Kwa upande wa nafasi ya mweka hazina wa klabu hiyo, ilichukuliwa na Namana Kabeza, baada ya kupata kura 50 na mbili kuharibika.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa ni Fedina Mwampwenge, Andrew Mlay, Ahmed Hussen, Mariamu Amiri, Mwenyimbegu Seleman, Said Haji, Tabu Mwalimu na Abdallah Masud.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.