Vipimo sahihi nguzo ya ushindani wa soko EAC

Mtanzania - - Biashara - Na LEONARD MANG’OHA -DAR ES SALAAM

WAKALA wa Vipimo (WMA), umesema ili wajasiriamali wa Tanzania waweze kushindana kibiashara katika soko la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, lazima wazingatie vipimo sahihi katika bidhaa zao.

Akizungumza katika maonyesho ya wajasiriamali Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Kaimu Meneja Sehemu ya Elimu, Habari na Mawasiliano, Iren John, alisema hatua hiyo itawasaidia wafanyabiashara wa Tanzania kuaminiwa na walaji wa nchi nyingine kwa kuwauzia bidhaa zinazoendana na thamani ya fedha zao.

Alisema katika maonyesho hayo maalumu kwa wanawake wajasiriamali, WMA inatoa elimu juu ya umuhimu wa matumizi ya vipimo sahihi ili baadaye waweze kushindana kwa haki katika soko la Afrika ya Mashariki.

Alisema ili wajasiriamali waweze kwenda sambamba na hitaji la Serikali ya Viwanda, wajasiriamali wadogo lazima watoke hapa walipo wahakikishe bidhaa zote wanazozalisha zinakuwa na ujazo halisi unaokubalika kimataifa.

“Ushiriki wetu katika maonesho hayo unalenga kuwawezesha wajasiriamali kufahamu umuhimu wa vipimo sahihi, kuweka maelezo ya biashara kwenye vifungashio vya bidhaa ikiwa ni pamoja na jina la utambulisho wa biashara wanayofanya.

“Mengine ni mahali wanapofanyia biashara pamoja na mawasiliano kwa kutumia lugha inayoeleweka katika eneo analofanyia biashara na kiasi halisi cha bidhaa.

“Kwa mfano, hapa wakati Waziri wa Viwanda na Biashara (Charles Mwijage), anawatembelea wajasiriamali, wako ambao amekuta wamefunga bidhaa ambazo wanadai kuwa ni gramu 500 lakini tunapoipima tunabaini kuwa imezidi uzito ulioandikwa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.