Ray C: Subirini burudani

Mtanzania - - Burudani - Na JENNIFER ULLEMBO

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, ameanza kujipanga kuandaa kazi nyingine baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu.

Akizungumza jana, Ray C alisema hivi sasa amerejea vema katika ubora wake, hivyo yupo tayari kuwapa mashabiki burudani ya kutosha.

Alisema baada ya kurudi na wimbo wake wa Unanimaliza ambao umeonyesha namna mashabiki wanavyomkubali, ameahidi kutoa kitu kipya.

“Mashabiki wanataka kusikia kitu kipya kutoka kwangu, nimeanza maandalizi kuhakikisha naenda nao sawa kwa kuwapa burudani zaidi na zaidi,” alisema Ray C.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.