10 wakata tiketi ya Beijing Shindano la Vipaji vya Sauti

Mtanzania - - Burudani - Na MWANDISHI WETU

WAshindi 10 watakaoenda kufanya kazi ya kuingiza sauti kwenye filamu za Kichina mjini Beijing, China, wamepatikana katika fainali ya Shindano la Star Times Vipaji vya Sauti lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Fainali ya shindano hilo la Star Times Vipaji vya Sauti, ilifanyika kwenye ukumbi uliomo ndani ya jengo jipya la Millenium Tower, Dar es Salaam baada ya kufanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Zanzibar kisha jumla ya washiriki 25 kupatikana kwa ajili kukamilisha zoezi hilo la kupata washindi 10 wa kwenda China. Washindi hao 10 watakaoenda China kufanya kazi ya kuingiza sauti kwenye filamu, ni mwigizaji Coletha Raymond, Hosea Joel, Bakari Hassan, Alex Herbert, Doreen Ponera ‘Pipi’, Hamza Tambwe, Jackline Shuma, Ally Ahmed, Mathias Komba na Mustafa Mussa. Fainali hiyo iliongozwa na majaji Mrisho Mpoto, Jacob Steven ‘JB’ na Jaji Mkuu Hilda Malecela, mmmoja wa washindi wa shindano la mwaka jana huku likipambwa na Mshehereshaji Silvery Mjuni ‘Mpoki’.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.