Tulia Traditional Dances Festival yazinduliwa

Mtanzania - - Burudani -

Na MWANDISHI WETU NAIBU Spika, Dk. Tulia Ackson, amezindua tamasha la ‘Tulia Traditional Dances Festival 2018’, huku akiwaomba wadau waliomsaidia katika tamasha lililopita kumpa ushirikiano. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Dk. Tulia alisema lengo la kuanzisha tamasha hilo ni kuona Watanzania wanauenzi utamaduni wao. “Mwaka huu tulipofanya tamasha hili tuliwapata washiriki kutoka mikoa 17, wakati mwaka jana walitoka katika mikoa miwili tu. Wabunge nao walitusaidia kuleta makundi kutoka katika majimbo yao,” alisema Dk. Tulia. Aliwashukuru wadau wote pamoja na vyombo vya habari kwa kushiriki katika tamasha hilo.

“Tunawashukuru sana wadau wote ambao tulishirikiana nao katika tamasha lililopita, watusaidie tena katika tamasha tunalotarajia kulifanya mwaka 2018 na lengo la kufanya haya ni kuhakikisha nchi yetu inaheshimu utamaduni wetu,” alisema Dk. Tulia.

Aliyataka makundi ambayo yatashiriki katika tamasha lijalo kujiandaa ili waweze kushindana na wenzao.

“Katika tamasha lililopita tuligawa pikipiki kumi na wale wa mikoani tuliwapatia fedha taslimu ya pikipiki,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.