FAO yaeleza watu wanavyofariki kila mwaka

Mtanzania - - Kanda - Na MWANDISHI WETU

“Kazi kubwa ya FAO kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Shirika la Wanyama Duniani (OIE) ni kuhakikisha matumizi mazuri ya dawa za viua sumu inatumika vema katika makundi yote matatu kwa maana ya binadamu, mifugo na mimea,” alisema Rubegwa.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara ya Kilimo na Mifugo, Selina Lyimo, alisema kwa sasa ni vigumu kutibu magonjwa yaliyopo kutokana na usugu wa vimelea.

SHIRIKA la Chakula Duniani

(FAO), limesema watu 700,000 hupoteza maisha duniani kila mwaka kutokana na matumizi ya dawa za viua sumu.

Pamoja na idadi hiyo, FAO limesema vifo hivyo vinatarajiwa kuongezeka hadi kufikia milioni 10 kila mwaka, ifikapo mwaka 2050 kama hakutakuwa na jitihada za kudhibiti dawa hizo.

Taarifa hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Mratibu wa Taifa wa Mradi wa Fleming Fund unaopambana na usugu wa vimelea vya magonjwa, Bachana Rubegwa, alipokuwa akizungumza katika semina ya waandishi wa habari.

Katika maelezo yake, Rubegwa alisema matumizi ya dawa hizo hayafai katika mimea na mifugo na kwamba wananchi wanatakiwa kuachana nazo ili kuepuka madhara makubwa zaidi yanayoweza kutokea.

Semina hiyo ilishirikisha pia wadau mbalimbali kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa (TFDA), Wizara ya Kilimo Zanzibar na wasomi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha (SUA) na wengine kutoka ofisi ya Msajili wa Baraza la Vetenary Tanzania (VCT).

Kwa mujibu wa Rubegwa, usugu wa vimelea vya magonjwa vimekuwa ni janga la kitaifa, hivyo wananchi wanapaswa kuepuka matumizi hayo ya dawa.

Hatutakuwa nyuma kumpongeza Rais kwa kuwa amesaidia kupambana na wezi – Ngiboli Ngilepoi

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.