Kampuni ya jasi China kuwekeza Dola milioni 200 kiwanda Kibaha

Mtanzania - - Biashara Na Uchumi - Na LEONARD MANG’OHA

KAMPUNI ya kichina ya (BNBM) kuwekeza zaidi ya Dola milioni 200 kuzalisha vifaa vya ujenzi nchini eneo la Kibaha. “Baada ya utafiti wa kina tuliamua kufanya uamuzi wa kuanzisha kiwanda kikubwa cha vifaa vya ujenzi na kuanzisha kituo cha utafiti na maendeleo ambacho kitaweza kusaidia kuhamisha ujuzi kwa Watanzania ambao watakuwa na uwezo wa kushiriki katika uzalishaji vifaa hivyo vya ujenzi” anasema Wang.

Kampuni hiyo pamoja na maeneo mengine inatarajia kujikita zaidi katika uzalishaji wa jasi (Gypsum) na unga wake.

Kujengwa kwa kiwanda hicho kitasaidia nchi nyingi za Afrika kwa kurahisisha upatikanaji wa vifaa vya ujenzi. BNBM ni miongoni mwa kampuni kubwa 500 wanachama wa mtandao wa Global Fortune ikiwa na uwezo wa kuzalisha mita za mraba bilioni 2.1 za jasi kwa mwaka.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Geoffrey Mwambe anasema kituo hicho kinaendelea kulifanya suala la kuvutia uwekezaji wa viwanda kama eneo muhimu na la kipaumbele.

“TIC inalenga kuvutia uwekezaji zaidi katika sekta ya viwanda ili kuongeza uzalishaji wa viwanda vya ndani ambavyo vitatoa masoko kwa malighafi zetu, kupunguza uingizaji wa bidhaa kwa gharama kubwa” anasema Mwambe.

Mwambe anasema atamhakikishia mwekezaji aliye tayari kuanzisha miradi mbalimbali nchini pamoja na kujenga mazingira mazuri ya kufanya biashara nchini na kuhamasisha wawekezaji wa ndani na wa nje kutambua maeneo ya uwekezaji.

Kwa mujibu wa TIC Tanzania inaendelea kufanya vizuri kiuwekezaji dhidi ya nchi za nyingine za Afrika Mashariki.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.