Polisi wajipanga kukabili wakimbizi

Mtanzania - - Kanda - Na SHOMARI BINDA

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya limejipanga kukabiliana na kuzuia watu wanaotaka kuingia nchini bila kufuata taratibu na sheria za kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya, Hennry Mwaibambe alikuwa akizungumza baada ya mazoezi ya polisi wa kanda hiyo na kushiriki usafi wa mazingira wa kila mwisho wa mwezi.

Alisema uzoefu unaonyesha yamekuwapo matukio ya watu kuingia nchini bila kufuata taratibu na kwa sasa wamejipanga katika kuzuia hali hiyo.

Mwaibambe alisema kuhama kutoka nchi moja kwenda nyingine zipo taratibu zinazopaswa kufuatwa.

Alisema wakati wa uchaguzi mkuu wa Kenya Agosti mwaka huu yalikuwapo matukio ya wizi wa mifugo ya wananchi.

“Tumejipanga vizuri katika mpaka wa Sirari katika kipindi hiki kuzuia wale wanaoingia nchini bila kuzingatia taratibu za sheria. “Mazoezi haya tuliyofanya ni utaratibu tuliojiwekea kama jeshi la polisi katika kujiweka vizuri.

“Sisi kama kanda maalumu tunataka kubadilisha utaratibu wa kufanya mazoezi ya pamoja mara mbili kwa mwezi.

“Lakini nitoe wito kwa askari wote kila mmoja kujitahidi kufanya mazoezi kila muda unapokuwa umepatikana,”alisema Mwaibambe.

Askari hao pia walishiriki kufanya usafi wa mazingira wa kila mwisho wa mwezi kwenye maeneo mbalimbali ikiwamo Hospitali ya Wilaya ya Tarime na kutoa msaada kwa wagonjwa waliolazwa kwenye hospitali hiyo.

Misaada hiyo ni pamoja na sabuni za kufulia, mafuta na dawa za meno.

Tumejipanga katika mpaka wa Sirari kuzuia wale wanaoingia nchini bila taratibu za sheria –Hennry Mwaibambe

MAJI: Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko, akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Kijiji cha Rogati, Kata ya Kemondo mkoani Kagera juzi, baada ya kuzindua visima vitatu vya maji safi vilivyotolewa na TPA kwa...

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.