RC awapa siku 30 wavuvi kujisajili

Mtanzania - - Kanda - Na RENATHA KIPAKA

MKUU wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenereli mstaafu, Salum Kijuu ametoa siku 30 kwa wavuvi mkoani hapa kujisajili katika idara zinazohusika kabla ya hatua kali hazijachukuliwa dhidi yao.

Alisema hatua hiyo inalenga kukomesha vitendo vya uvuvi haramu na kudhibiti kasi ya kupungua samaki katika ziwa Victoria.

Alisema alisema katika usajili huo wavuvi watatakiwa kuainisha aina uvuvi wanaoufanya na wanautekeleza kwa kutumia vifaa vya aina gani.

“Tunataka wavuvi wajisajili tubaini kila mvuvi anavua kwa namna gani na anatumia kifaa gani na hatua hii itaendeshwa kwa mwezi mmoja.

“Kwa yeyote atakayeleta mgomo katika katika hatua hii basi nitafanya operesheni kama niliyoifanya kwenye mifugo.

“Kwa sababu kwenye uvuvi kila siku tunateketeza nyavu na zana haramu lakini watu hawabadiliki, sasa adhabu itabadilika ili kuondoa mazoea,” alisema Kijuu.

Kaimu Ofisa Mfawidhi Uvuvi Doria Kanda ya Kagera, Gabriel Mageni, alisema ni vema doria ya kudhibiti uvuvi haramu ikaendelea bila mwingiliano wa siasa ili kufanikisha azma ya kutokomeza uvuvi haramu unaoathiri maisha ya viumbe hai wa majini.

Alizitaka halmashauri za wilaya zenye maeneo ya uvuvi kutenga asilimia 15 ya mapato ya uvuvi kufanya doria ikizingatiwa kwa sasa hakuna doria ya kutosha na iliyopo inafanyika kwa kiwango cha chini.

Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Ruyango, alisema ili kutokomeza uvuvi haramu ni vema serikali ikawadhibiti viongozi wa serikali za mitaa kwa sababu ndiyo wanaomiliki nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu.

“Inakuwa shida kufanikisha hatua hii wakati wamiliki wa vifaa vinavyosabanisha uharibufu wakati mwingine hushiriki katika vikao vya uamuzi vya kata.

Kwa sababu kwenye uvuvi kila siku tunateketeza nyavu na zana haramu – Salum Kijuu

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.