JPM atangaza kiama kwa wakuu wa mikoa wasiojenga viwanda

Mtanzania - - Mbele - JUDITH NYANGE Na BENJAMIN MASESE

RAIS Dk. John Magufuli amesema mkuu wa mkoa yoyote atakayeshindwa kupeleka wawekezaji kujenga viwanda katika mkoa wake hatamvumilia.

Amewataka wakuu wote wa mikoa kuiga mfano wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, ambaye amekaribisha wawekezaji wanaojenga viwanda vipya.

Agizo hilo alilitoa Mwanza jana alipokuwa akituhubia mkutano wa hadhara eneo la Nyakato wilayani Ilemela.

Rais alisema viwanda si mali yake bali ni mali ya wananchi ambao ndiyo walipa kodi.

Alisema ingawa Tanzania ilikuwa na viwanda vingi, hivi sasa Watanzania wamebaki hawapati majibu vilikwenda wapi hali inayoifanya Serikali iamue kufanya kazi ya kuvifufua vya zamani na kujenga vipya.

Kabla ya kuhutubia mkutano huo Rais alizindua kiwanda cha vinywaji baridi cha Sayona kilichojengwa Nyakato. Leo anatarajiwa kuzindua viwanda vingine viwili.

Alisema amefurahishwa na ahadi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela na kwamba kila anapopita ndani ya mkoa huo, lazima huzindua kiwanda ama viwanda kwa vile wawekezaji wengi hukimbilia kuwekeza mkoani humo.

“Nataka nichukue fursa hii kukupongeza mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa kuwatafuta wawekezaji wengi na kuwekeza kwenye viwanda.

“Nataka wakuu wa mikoa wa aina hii, mkuu wa mkoa ambaye kila siku napita mkoa wake bila kuzindua kiwanda sitamvumilia kufanya naye kazi, lazima ang’oke.

“Mkuu wa Mkoa ambaye haleti wawekezaji katika mkoa wake kujenga viwanda… kwanza hivyo viwanda si vya wakuu wa mikoa bali ni mali ya wananchi. Kuwapo viwanda kutasaidia kutengeneza ajira, hayo ndiyo maendeleo tunayotaka. “Haiwezekani Tanzania iwauzie … tulime pamba tuwauzie wazungu watengeneze nguo wazivae kisha kutuletea zikiwa mitumba.

“Tunataka nguo zitengenezwe hapa na Mwatex ili ziuzwe kwa bei nafuu kuliko hiyo mitumba. Sizuii mitumba lakini nguo mpya na bora lazima zitengenezwe hapa,” alisema Rais Magufuli.

Alimweleza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, ajirekebisha na afanye kazi ya kufufua, kufunga na kuchukua viwanda visivyofanya kazi na awape watu wengine.

“Haiwezekani unapewa kiwanda kutoka mwaka wa kwanza hadi wa 20 bila uzalishaji, wenye viwnada hivyo virudisheni haraka kwa sababu tutakapoanza kuwashika tutadai faida ambayo walikuwa wakiipata miaka hiyo,” alisema.

MGOGORO WA MEYA

Akizungumzia suala la mgogoro wa Meya, Rais Magufuli alisema ameyaona mabango likiwamo lililokuwa limeandika kuwa Meya wa jiji la Mwanza, James Bwire, amewekwa ndani na Mkuu wa Mkoa ili asionane na rais ingawa alikuwa ameachiwa huru.

Rais Magufuli aliwataka viongozi wa Mwanza kuacha malumbano na kukaa meza moja kumaliza mambo yao kwa kuwa wanatoka chama kimoja. Alisisitiza kwamba wakiendelea na tabia hiyo hawatafika popote.

“Mkiendelea kulumbana mtashindwa kutatua kero za wananchi, haya mabango ya mara kwa mara yanatokea kwa sababu

PICHA: IKULU

Rais Dk. John Magufuli na mkewe Janeth Magufuli, wakiwapungia mkono wananchi waliopo chini ya Daraja la Furahisha baada ya kulizindua jijini Mwanaza jana.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.