Madaktari kutoka Muhimbili

Mtanzania - - Kanda -

MADAKTARI bingwa 27 wa kliniki tembezi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam, wamekwisha kuwahudumia wagonjwa 429 wa magonjwa mbalimbali waliojitokeza kutibiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Kagera, anaripoti Renatha Kipaka.

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Kagera, Felix Otieno alisema tangu kuanza kliniki hiyo Novemba 5 mwaka huu tayari wamesajiliwa wagonjwa 858.

Otieno alisema madaktari hao watakaokuwapo mkoani Kagera kwa siku tano wanatarajia kutibu wagonjwa 4,000 hadi 5,000.

Mgeni rasmi katika ufunguzi wa kliniki hiyo tembezi, Kaimu Mkuu wa Mkoa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Luyango alisema madaktari hao ni kwa ajili ya wagonjwa wa moyo, kinywa, meno, tezi dume, mifupa na magonjwa ya watoto.

MATREKTA: Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia) akikabidhi ufunguo wa trekta kwa mmoja wa viongozi 24 wa vyama vya ushirika vya msingi na masoko (AMCOS) vya mikoa ya Kanda ya Ziwa waliokopeshwa matrekta yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 1.5 yaliyotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). Wanaoshuhudia ni Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine. – PICHA: MPIGAPICHA WETU

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.