MIAKA MITATU YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO: SEKTA YA HIFADHI YA JAMII YENYE SURA TOFAUTI

Mtanzania - - Tangazo -

MOJA ya eneo nyeti kwa watanzania ambalo Serikali ya awamu ya tano chini ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeliwekea msisitizo ni kuwa na Mfumo wa Hifadhi ya Jamii imara na endelevu kwa maisha ya wanachama hasa wanapopoteza uwezo wa kufanyakazi, huku mchango wake kwa maendeleo ya taifa ukizidi kukua siku hadi siku.

Serikali kupitia Mamlaka ya Msimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imefanya maboresho mbalimbali kuhakikisha wanachama zaidi ya milioni 2.4 wanajiunga na Mifuko ya Pensheni; Kaya milioni 2.2 zinajiunga na Mifuko ya Afya ya Jamii (CHFs) ambapo jumla ya wategemezi milioni 16 wananufaika na huduma za Hifadhi ya Jamii na wanapata kinga dhidi ya majanga mbalimbali yatokanayo na uwezo wa kufanyakazi kama vile maradhi, ulemavu, kifo au kustaafu.

Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya tano katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii ni Pamoja na; Kupunguza gharama za uendeshaji toka wastani wa asilimia 19 mpaka asilimia 8; kuboresha mafao ya pensheni kutoka kikotoo cha asilimia 67 hadi asilimia 72.5; kuthaminisha pensheni na kuongeza kima cha chini cha pensheni toka shilingi 50,000/- hadi shilingi 100,000/- kwa mwezi; kulipa deni la michango shilingi trilioni 1.3 na kuandaa fao la upotevu wa ajira pamoja na kuboresha fao la warithi.

Katika kipindi cha miaka mitatu cha serikali ya awamu ya tano, moja ya mafanikio ni mabadiliko ya sheria ya hifadhi ya jamii ambayo ilianza kufanyakazi Agosti mosi, mwaka huu, ikiwa na maboresho kwenye maeneo muhimu yanayogusa maisha ya wanachama moja kwa moja.

Sheria hiyo imeunganisha mifuko ya PPF, GEPF, PSPF na LAPF na kuunda Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF ambao unahudumia watumishi wa Umma na Mfuko wa NSSF unaohudumia sekta binafsi pekee, huku mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) ukiendelea na majukumu yake ya kutoa Bima ya afya kwa Watanzania na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa fidia za kuumia kazini. BIMA YA AFYA YA JAMII Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Dkt. Irene Isaka, anaelezea mafanikio ya sekta ya hifadhi ya jamii kwa Miaka Mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano kuwa ni pamoja na mamlaka kusimamia mfuko wa NHIF na kusajili Mifuko ya Bima ya Jamii (CHF) ili huduma za Afya iwafikie Mwananchi katika ngazi za Halmashauri.

“Katika kutekeleza azima hii, SSRA imesajili jumla ya Mifuko ya CHF 166 kufikia Juni, 2018, sambamba na kuendesha zoezi hilo la usajili, SSRA imeendesha mafunzo ya usimamizi na utoaji wa huduma za bima ya afya kwa Watendaji wa Halmashauri 166 nchini,” anasema.

Aidha, anasema hatua hizi zimesaidia kuongeza wigo wa huduma ya afya ya jamii kutoka kaya 1,452,855 (Juni 2015) hadi kufikia kaya milioni 2.2 (Juni 2018). Anasema pia hifadhi ya jamii inahamasisha wanachama kujiunga na huduma za Bima ya Afya na Mifuko ya Hifadhi za Jamii ili kujihakikishia kinga dhidi ya majanga na maisha ya uzeeni na baada ya kustaafu. SKIMU ZA HIYARI, FAO LA KUKOSA AJIRA Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu, SSRA imewezesha Mifuko ya Pensheni kuanzisha skimu za hiyari ili kuwafikia wananchi wakiwemo wajasiriamali na vijana kwenye sekta isiyo rasmi kama vile Wakulima Scheme, Boda Boda Scheme, Wavuvi Scheme, Madini Scheme, Mashambani, Mama Lishe na Toto Card.

Aidha, anasema SSRA imejikita katika kuhamasisha vijana na wajasiriamali wadogo kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii, kwa kuwaelimisha faida za kuwa mwanachama wa mfuko, manufaa yaliyopo ikiwamo mafao ya matibabu, mikopo na umuhimu wa kuweka akiba ambayo itasaidia uzeeni. FAO LA UZAZI Dkt. Irene Isaka anasema katika kuhakikisha kundi la Wanawake nao wanashiriki na kunufaika na huduma za hifadhi ya Jamii, Sheria ya PSSSF na NSSF inatoa fao la uzazi, na kwa mujibu wa takwimu wanawake 17, 392 wamenufaika na fao hilo, na kwamba kwa kipindi kinachoishia Machi 2018, takribani shilingi Bilioni 26 zimelipwa na Mifuko kwenye fao la uzazi.

Kwa mujibu wa Dkt. Irene Isaka, anasema Sheria Mpya imepanua wigo wa fao la uzazi ili kujumuisha huduma za matibabu kwa mzazi kabla na baada ya uzazi, jambo ambalo litasaidia wazazi wengi na hivyo kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

“Jumla ya wanawake wachangiaji katika Mifuko ya Hiafdhi ya Jamii kufikia Machi, 2018 ni 476,114 na wastani wa wastaafu wanawake ni 33,441 ambao wanapokea pensheni,” anafafanua.

mifuko ya PPF, GEPF, PSPF na LAPF na kuunda Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF ambao unahudumia watumishi wa Umma na Mfuko wa NSSF unaohudumia sekta binafsi pekee, huku mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) ukiendelea na majukumu yake ya kutoa Bima ya afya kwa Watanzania na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa fidia za kuumia kazini.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.