Mafanikio ya mwanafunzi yapo mikononi mwa wazazi

Mtanzania - - Tahariri - Na MWANDISHI WETU

USHIRIKI wa wazazi katika mchakato wa ujifunzaji wa watoto ni suala lisilo na mjadala. Matokeo ya tafiti mbalimbali zilizofanyika hapa nchini yanasisitiza kuwa wazazi wanaposhirikiana na walimu inakuwa rahisi kwa mtoto kupata mafanikio yanayotarajiwa.

Hali halisi inaonesha wazazi wengi hawajajenga desturi ya kushirikiana kwa karibu na walimu. Wazazi wamewaachia walimu kazi ya kuhakikisha mtoto anafaulu.

Huwa wanasubiri mwisho wa muhula kupata matokeo mazuri ya mitihani. Matokeo hayo ndiyo yanayotumika na wazazi kutathmini kazi inayofanywa na walimu ili kufanya uamuzi wa ama kulipa kiasi cha ada kinachotakiwa kwa muhula unaofuata au kutafuta shule nyingine inayojua wajibu wake. Ingawa ni kweli mwalimu ana nafasi yake katika kumwezesha mtoto kujifunza, sehemu kubwa ya kazi inabaki kuwa ya mzazi mwenyewe.

Zoezi la mtoto kujifunza halianzii shuleni. Mzazi ndiye mwalimu wa kwanza mwenye wajibu wa kuweka mazingira sisimushi nyumbani yatakayomsaidia mtoto kufyonza maarifa hatua kwa hatua. Kwa mfano, mzazi ndiye mwenye jukumu la kuhakikisha mwanawe anapenda kusoma. Inapotokea mzazi hajamjengea mwanawe tabia ya kupenda kusoma, mwalimu atakayempokea mtoto huyu shuleni atakuwa na kazi ya ziada ya kufanya kufidia kazi muhimu ambayo haikufanyika nyumbani.

Lakini pia, mwalimu anayetarajiwa kufidia upungufu wa kimalezi ulioanzia nyumbani, naye kwa upande mwingine anakabiliana na changamoto nyingi ikiwamo idadi kubwa ya wanafunzi. Kinadharia, mwalimu analazimika kumfahamu kila mwanafunzi si tu kwa jina lake, lakini hata kufahamu mahitaji yake ya kibinafsi yanayomwezesha kujifunza vizuri. Idadi kubwa ya wanafunzi anayokuwa nayo mwalimu inafanya kazi hii nyeti isiwezekane. Katika mazingira kama haya, mzazi anapotambua wajibu wake na kusaidiana na mwalimu anakuwa sehemu ya suluhisho.

Mambo kadhaa yanaweza kufanyika. Weka mazingira sisimushi nyumbani yanayomkuza mtoto kiufahamu, kimwili, kimahusiano, kimaadili na kiroho. Ili hilo liwezekane, hakikisha unajenga ukaribu na mtoto tangu anapozaliwa. Tenga muda mfupi kwa siku kuzungumza na mwanao. Mfanye

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.