Serikali kujenga magereza 52

Mtanzania - - Kanda -

WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema ina mpango wa kujenga magereza 52 katika maeneo tofauti.

Hayo yalielezwa jana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo,Hamadi Masauni alipojibu swali la Mbunge wa Rorya, Lameck Airo (Pichani) (CCM).

Katika swali lake, mbunge huyo alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kujenga gereza la Wilaya ya Rorya.

Akijibu swali hilo, Masauni alisema Serikali ina mpango wa kujenga magereza 52 katika maeneo tofauti likiwamo eneo la Rorya lakini changamoto kubwa ni upatikanaji wa fedha.

Alisema Wilaya ya Rorya ni miongoni mwa wilaya 52 nchini zisizo na magereza.

“Ni azma ya Serikali kujenga magereza katika maeneo mbalimbali nchini ikiwamo Wilaya ya Rorya,”alisema.

Alisema kutokana na ufinyu wa bajeti Serikali itaendelea kukamilisha magereza ambayo ujenzi wake umekwisha kuanza.

Alisema kipaumbele ni kuhakikisha inakamilisha miradi ambayo ipo katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.