Visa, Halopesa waja na malipo ya QR kwa wateja

Mtanzania - - Biashara - Na MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya teknolojia ya malipo ya kimataifa ya Visa, imetangaza ushirikiano wa mkakati na Halotel ili kuwezesha malipo ya Visa kwenye simu kwa kutuma codi ya QR kwa wateja wa Halotel nchini.

Huduma hiyo itatolewa mwanzoni mwa mwaka 2019 na hivyo kuwezesha wateja zaidi ya milioni moja wa HaloPesa kutumia Visa kwenye simu ili waweze kufanya malipo ya biashara kwa salama na kuweka na kutoa fedha kwa mawakala wa Visa. Hatua hiyo itamwezesha mteja yeyote wa HaloPesa, ikiwa ni pamoja na wale ambao hawana akaunti ya benki, kufaidika na huduma hiyo.

Akizungumzia hatua hiyo, Meneja Mkuu wa Visa wa Afrika Mashariki, Kevin Langley, alisema lengo la huduma hiyo ni kuunganisha Watanzania zaidi kwenye mfumo wa malipo ya kimataifa, kuleta huduma ya malipo ya Visa ya usalama na urahisi kwa watumiaji na wafanyabiashara.

“Tunafurahia ushirikiano huu na mojawapo wa kampuni maarufu ya simu ya Halotel. Ushirikiano wetu na Halotel utahakikisha kuwa Watanzania wanaweza kufanya malipo ya QR kwa kutumia Visa kwenye simu zao kwa wauzaji na wafanyabiashara zaidi ya 40,000.

“Pia itasaidia kuongeza ushirikishaji wa kifedha kwa watumiaji ambao sasa wataweza kufaidika na kushiriki katika mfumo wa eco Visa,” alisema.

Halotel ni kampuni ya simu inayokua kwa haraka zaidi nchini Tanzania, ambayo ilianzishwa mwaka 2015, ambapo ndani ya miaka mitatu imepata wateja zaidi ya milioni nne na zaidi ya milioni moja wanatumia huduma ya HaloPesa.

Pamoja na hali hiyo, pia kampuni inao wakala 40,000 kote nchini.

“Tunajivunia kushirikiana na Visa katika mpango huu. Kwa ushirikiano huu, tutaweza kuwa na uwezo wa kuletea wateja wetu huduma za kimataifa za malipo za Visa na kuwawezesha wateja wetu kulipia na kulipwa kwa urahisi zaidi,” alisema Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania, Nguyen Van Son.

Kupitia ushirikiano, HaloPesa itawapa watumiaji fursa ya kufanya malipo kutumia codi ya QR ya Visa hapa Tanzania na kote duniani.

– .PICHA:LOVENESS BERNARD

MAZUNGUMZO: Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB), Jaji Thomas Mihayo, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi kuhusu kushiriki katika maonesho ya CIIE ya China, WTM ya Uingereza na ‘roadshow’ nchini China mwezi huu. Kushoto ni Meneja Masoko na Usambazaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Edward Nkwabi ambaye alitangaza kuzinduliwa kwa safari ya China kupitia Bangkok kwa ndege ya shirika hilo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.