Kiongozi wa zamani aongoza matokeo ya awali urais

Mtanzania - - Kimataifa / Matangazo -

SHUGHULI za kuhesabu kura katika uchaguzi wa rais iliendelea Madagascar jana huku kiongozi wa zamani Andry Rajoelina akiongoza kwa ushindi mdogo katika matokeo ya awali kutokana na idadi ndogo ya vituo vya kupigia kura.

Matokeo ya awali kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) yaliyotolewa mapema jana kutoka karibu vituo 100 vya kupigia kura kati ya 24,000 yalionyesha Rajoelina akiwa mbele ya wagombea wengine wawili, akiwa na asilimia 44.4 ya kura. Uchaguzi huo uliwakutanisha Rajoelina na Rais wa sasa, Hery Rajaonarimampianina, ambaye anawania muhula wa pili madarakani na kiongozi mwingine wa zamani, Marc Ravalomanana.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.