Timu 16 kushiriki Afrika Mashariki mikono

Mtanzania - - Michezo - Na IBRAHIM MAKAME

JUMLA ya klabu 16 zinatarajiwa kushiriki mashindano ya Afrika Mashariki mpira wa mikono, Jumapili ijayo kwenye viwanja vya Jeshi Nyuki, visiwani Zanzibar.

Akizugumza na waandishi wa habari jana visiwani hapa, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Mikono Zanzibar (ZAHA), Salum Hassan Salum, alisema kwa sasa hatua inayoendelea ni kuwapokea wageni kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki, ikiwemo DRC Congo, ambao watawakilishwa na timu nne, huku Kenya ikitarajiwa kuwakilishwa na timu sita.

Alisema chama hicho tayari kimeshajiandaa kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika, licha ya kuwa baadhi ya nchi zinasuasua kuleta timu.

“Sisi kama ZAHA upande wetu tutagharamikia usafiri na malazi, baadhi ya gharama zinakuwa chini ya Shirikisho la Mpira wa Mikono Afrika (CAHB),” alisema Salum.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.