Daba waomba mchango wa milioni mbili

Mtanzania - - Michezo - Na WINFRIDA MTOI

CHAMA cha Ngumi za Ridhaa Mkoa wa Dar es Salaam (Daba), kimewaomba wadau wa mchezo huo kuwachangia kiasi cha Sh milioni mbili ili kiweze kuendesha mashindano ya Klabu Bingwa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, mwenyekiti wa Daba, Akaroly Godfrey (pichani), alisema mashindano hayo yalitakiwa kufanyika wiki iliyopita, lakini imeshindikana baada ya kukosekana kwa fedha.

Alisema kuwa, timu zilikuwa zimeshafanya mazoezi na ratiba ilikuwa imepangwa, wakahairisha dakika za mwisho, kutokana na kukosa fedha za kuhudumia mabondia wakati wa mashindano.

“Tuliandaa bajeti muda mrefu, tukapeleka katika kampuni mbalimbali kuomba udhamini, lakini hadi sasa hakuna tulichopata, tunawaomba wadau wa michezo kutuchangia ili tufanikishe mashindano haya,” alisema Godfrey.

Godfrey alisema malengo yao ni kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kabla ya mwaka huu kumalizika.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.