Serengeti Boys, Yanga B kujipima

Mtanzania - - Michezo - Na WINFRIDA MTOI

TIMU ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, inatarajia kuvaana na Yanga B katika mchezo wa kirafiki uliopangwa kufanyika kesho kwenye Uwanja wa Karume jijini hapa.

Serengeti Boys ipo kambini katika hosteli za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ikijiandaa na michuano ya nchi za Kusini mwa Afrika (Cosafa), itakayoanza Desemba 6-20, mwaka huu nchini Botswana.

Akizungumza na MTANZANIA, kocha msaidizi wa kikosi hicho, Maalim Saleh ‘Romario’, alisema wameomba mechi hiyo kwa lengo la kupima kiwango cha wachezaji hao, baada ya mazoezi ya wiki mbili.

“Tangu tumeingia kambini ni wiki ya pili, hatujacheza mchezo wowote wa kirafiki, tunatarajia kuanza wiki hii, tunashukuru wachezaji wote wapo katika hali nzuri hakuna majeruhi,” alisema Romario.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.