CBA, M-pawa kunufaisha wanyonge

Mtanzania - - Biashara - NA MWANDISHI WETU

BENKI ya Biashara Afrika (CBA) kwa ushirikiano na Kampuni ya Simu ya Vodacom imezidua promosheni maalumu ya kuwapa faida mara mbili wateja wote wanaotumia huduma ya kampuni hiyo ya M-Pawa.

Promosheni hiyo iliyoanza Novemba Mosi hadi Desemba 13, imelenga kutoa Sh milioni 10 kwa mteja ambaye ataibuka mshindi wa droo ya wateja wote wa huduma ya M-pawa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa CBA nchini, Julius Konyani alisema promosheni hiyo imelenga kuwanufaisha wateja wote wa huduma ya M-pawa ambao wanakopa fedha na kurejesha kwa wakati.

Alisema mbali na droo ya Sh milioni 10, pia washindi wengine watano watapatiwa zawaidi ya bajaji kwa kila mmoja. Konyani alisema promosheni hiyo ambayo inakwenda kwa jina la “Shinda na M-pawa” itawanufaisha wateja wengine 200 kila wiki kwa kuwapatia zawadi mbalimbali.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.