Wahitimu mafuzo TBL watunukiwa vyeti

Mtanzania - - Biashara - NA MWANDISHI WETU

WASHIRIKI 167 wanaofanya biashara kwa kushirikiana Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) walioshiriki mafunzo ya ujasiriamali na mbinu za biashara yanayojulikana kama Retail Development Programme (RDP), jana walitunukiwa vyeti katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Wanufaika wa mafunzo haya, ambao wengi wao ni wamiliki wa mabaa, mameneja wa baa na wafanyakazi, wametokea katika Wilaya za Temeke, Kinondoni, Kigamboni, Ilala Ubungo na yaliendeshwa na TBL chini ya kampuni mama ya ABIn Bev.

Mkurugenzi wa ukuzaji wa Masoko wa ABIn Bev, Kanda ya Afrika Mashariki, Carlos Bernitt, aliwapongeza wahitimu wa mafunzo hayo.

“Nawapongeza kwa kuhitimu mafunzo haya na nina imani mkitumia vizuri maarifa mliyoyapata yatawasaidia kukuza biashara zenu na kuleta maendeleo ya kwenu binafsi na jamii nzima kwa ujumla,” alisema Bernitt.

Akizungumza kuhusu mafunzo hayo, Meneja Masoko na Ukuzaji Biashara wa TBL, Edith Bebwa, alisema mafunzo ya ujasiriamali yanayotolewa chini ya mpango unaojulikana kama Retail Development Programme (RDP), yanalenga kuwapatia mbinu za kufanya biashara kwa ufasaha wafanyabiashara wadogo wanaoshirikiana nao kibiashara ili

kuwasaidia kukua. “Mafunzo haya yameendeshwa na wataalamu wa masuala ya ujasiriamali na washiriki wamewezeshwa kujifunza mambo mbalimbali ya biashara, ikiwamo urasimishaji biashara zao, tunaamini yatawasaidia kufanya vizuri sambamba na malengo yetu yaliyokusudiwa,” alisema Bebwa.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo haya, Damas Asenga alisema kuwa, mafunzo haya yamewasaidia kujua masuala mbalimbali ya kuendesha biashara, hasa za kuuza vinywaji kama vile utunzaji wa hesabu, mbinu za kuongeza mauzo, huduma kwa wateja, nidhamu ya matumizi ya pesa, jinsi ya kukabiliana na ushindani wa kibiashara.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.