Kante mguu sawa Stamford Bridge

MZALENDO - - JILIWAZE - KIEV, Ukraine

BAADA ya kufanyiwa vipimo kuchunguza afya yake, N’Golo Kante anatarajiwa kusaini mkataba na Chelsea kuichezea timu hiyo wakati wowote. Taarifa za uhakika zinaeleza, Kante atamwaga wino kwa dau la pauni milioni 30 (Sawa na zaidi ya sh. Bilioni 75), kabla ya kuvaa uzi huo wa Stamford Bridge. Kwa mujibu wa mshambuliaji huyo, ambaye msimu uliopita aling’ara na Leicester City iliyotwaa ubingwa, juzi alimaliza kupimwa afya, mambo yatakuwa shwari Stamford Bridge. Kimsingi, hatua iliyobaki ni kusaini nyaraka za mkataba kisha kutangazwa rasmi kuwa ni mchezaji halali wa Chelsea. Wakati kocha wa Chelsea, Antonio Conte akiwa kwenye majukumu ya michuano ya Euro 2016, uongozi wa klabu hiyo, ulipambana kuhakikisha mfumania nyavu huyo anatua Stamford Bridge. Licha ya Kante kutarajiwa kusaini mkataba usiku, hatakuwa na mpango wa kuungana na wachezaji wenzake kwa sasa, mpaka baadae. Kante alikuwa na majukumu kwenye timu yake ya taifa wakati ya michuano ya Euro 2016. UKRAINE imemteua nyota wa zamani wa AC Milan na Chelsea, Andriy Shevchenko kuwa kocha mpya wa timu ya taifa hilo.

Shevchenko (39), aliyeichezea timu hiyo michezo 111, anachukua nafasi ya Mykhaylo Fomenko ambaye mkataba wake umemalizika baada ya timu hiyo kutolewa hatua ya makundi, michuano ya ulaya iliyochezwa Ufaransa.

Awali, Shevchenko alikuwa msaidizi wa Fomenko. Ukraine ilifungwa mechi zake dhidi ya Ujerumani, Ireland Kaskazini, na Poland.

Mchezaji huyo wa zamani wa Dynamo Kyiv, aliyestaafu soka mwaka 2012, hajawahi kufanya kazi ya ukocha kabisa.

Mbali ya kuifungia Ukraine mabao 48 Shevchenko alikuwa nahodha wa timu ya taifa hilo katika fainali za kombe la dunia mwaka 2006.

Amesaini mkataba wa miaka miwili, baadae unaweza kuongezwa na kufikia minne.

Aidha, beki wa zamani wa Italia, Mauro Tassotti, ambaye alikuwa kocha msaidizi wakati Shevchenko akiwa AC Milan, atajumuishwa kwenye benchi la ufundi akiwemo pia, kocha wa zamani wa Dynamo, Raul Riancho.

Mechi ya kwanza kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 2018, Ukraine itakuwa mwenyeji wa Iceland, Septemba mwaka huu.

Timu hizo ziko kundi la I na Croatia, Uturuki, Finland na Kosovo.

LONDON, England

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.