JPM ampa kazi Mrema

Pia ateua viongozi, watendaji wa taasisi za serikali Baadhi ya maofisa Jeshi la Polisi wapandishwa vyeo

MZALENDO - - MBELE - NA MWANDISHI WETU

RAIS Dk. John Magufuli, amemteua Augustino Mrema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia jana.

Pia, amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi za serikali na kuwapandisha vyeo maofisa 59 wa Jeshi la Polisi.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu, Gerson Msigwa, ilisema Rais Dk. Magufuli amemteua Mrema kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji mstaafu Eusebia Munuo ambaye muda wake umemalizika.

Wengine walioteuliwa na nafasi zao kwenye mabano ni Profesa William Mahalu (Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete).

Profesa Mohamed Janabi (Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete).

Profesa Angelo Mapunda (Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu).

Taarifa ilisema Rais Dk. Magufuli pia amemteua Sengiro Mulebya (Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu).

Oliva Mhaiki (Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC)).

Mwalimu Winifrida Rutaindurwa (Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC)).

Wengine walioteuliwa ni Dk. Charles Majinge (Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili).

Dk. Julius Mwaiselage (Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road). Uteuzi wa watendaji hao ulianza juzi na wengine jana.

Katika hatua nyingine, Rais Dk. Magufuli amewapandisha vyeo maofisa 25 wa Jeshi la Polisi.

Katika vyeo vya kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) walipandishwa ni Essaka Mugasa, Adamson Mponi na Charles Kenyela.

Wengine ni Richard Revocatus, Geofrey Kamwela, Lucas Mkondya, John Gubada, Matanga Mbushi, Frasser Kashai, Ferdinand Mtui, Germanus Muhume, Fulgence Ngonyani, Modestus Lyimo na Mboje Kanga.

Pia wapo Gabriel Njau, Ahmed Msangi, Anthony Rutashubulugukwa, Dhahir Kidavashari, Ndalo Shihango, Shaaban Hiki, Simon Chillery, Leonard Paul, Ahmada Khamis, Aziz Mohamed na Juma Ally.

Taarifa ilisema maofisa 34 waliopandishwa vyeo kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) ni Fortunatus Musilimu, Goyayi Goyayi na Gabriel Mukungu.

Wengine ni Ally Ally, Edward Bukombe, Sifael Mkonyi, Naftari Mantamba, Onesmo Lyanga, Paul Kasabago, Dadid Hiza, Robert Mayala, Lazaro Mambosasa, Mihayo Msikhela, Ramadhani Mungi na Henry Sikoki.

Renata Mzinga, Suzan Kaganda, Neema Mwanga, Mponjoli Lotson, Benedict Wakulyamba, Wilbroad Mtafungwa, Gemini Mushi, Peter Kakamba, Ramadhani Hassan, Christopher Fuime, Charles Ulaya, Gilles Muroto na Mwamini Lwantale.

Maofisa wengine ni Allute Makita, Kheriyangu Khamis, Nassor Mohammed, Salehe Salehe na Mohamed Mohamed ambao wamepandishwa vyeo kuanzia juzi

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.