Sumaye ni mfa maji -Bulembo

MZALENDO - - MBELE - NA THOMAS MTINGE

MWENYEKITI wa Taifa wa Jumuia ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo, amemfananisha Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye na mfa maji kutokana na kauli zake za kutapatapa za kuiombea mabaya CCM.

Alisema kauli ya Sumaye kudai kwamba Rais Dk. John Magufuli anaimarisha upinzani, hivyo CCM kuwa na nafasi finyu ya ushindi katika uchaguzi wa mwaka 2020 inaonyesha jinsi kiongozi huyo alivyofilisika kisiasa.

Bulembo alisema nchi yenye demokrasia na utawala bora, kamwe haiwezi kuongozwa kwa maandamano bali kwa misingi ya sheria.

Alisema maandamano yenye lengo la kukwamisha shughuli za maendeleo hayana tija na hayapaswi kufumbiwa macho na mtu yeyote yule.

ìKama huna kazi ya kufanya ni bora ukalale tu hata usiku na mchana na si kufanya mikutano ya maandamano kwa kisingizio cha kunyimwa haki kumbe huna kazi ya kufanya,î alisema Bulembo.

Juzi, baadhi ya vyombo vya habari vilimkariri Sumaye akisema kuwa kitendo cha Rais Dk. Magufuli kuzuia mikutano ya vyama vya siasa, kinaimarisha upinzani na kuifanya CCM kuwa na nafasi finyu ya ushindi mwaka 2020.

ìSumaye ni mfa maji anayetapatapaÖhaoni wapi pa kushika wala pa kukimbilia. Mara nyingi mfa maji hutokwa na maneno ya kila aina akijaribu kuokoa roho yake, lakini siku ikifika, imefika tu.”

ìSumaye baada ya kuona CHADEMA inazama, ameanza kutapatapa kwa kuiombea mabaya CCM akizani itapoteza umaarufu wakeÖmimi nasema, yeye na timu yake tukutane 2020 aone kilichomnyoa kanga manyoya,î alisema Bulembo.

Alisema katika uchaguzi wa mwaka 2020, CCM itakua gumzo kubwa kwa kuwa itakua imeshaimarisha safu yake ya uongozi katika ngazi zote tayari kujiandaa na uchaguzi huo dhidi ya kambi ya upinzani.

ìNamshangaa SumayeÖbadala ya kujadili hatima ya chama chake katika uchaguzi huo kuwa kitaanguka kwa staili ipi, anaijadili CCM. ìUmeona wapi mtu akicheza mpira akiwa nje ya uwanja. Sumaye yuko CHADEMA huu ujasiri wa kujua hatima ya CCM anaupata wapi kama si una i?î alihoji Bulembo.

Alisema Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki ijayo mjini Dodoma pamoja na mambo mengine, utaandaa kaburi la kuizika rasmi CHADEMA katika uchaguzi mkuu ujao.

ìTunakwenda Dodoma kujipanga upya. Tutaondoa makapi, wasaliti na kuinoa upya CCM. Macho na masikio ya Watanzania yatahamia Dodoma wakati huo wakitaka kujua CCM imejipanga vipi. Hakika maamuzi ya mkutano huo ndiyo yatakayoizika CHADEMA na wenzake,î alisema Bulembo ambaye amekuwa mwiba kwa wapinzani.

Alisema madhumuni ya chama chochote cha siasa ni kuongoza dola, hivyo CCM itahakikisha inazidi kujiimarisha ili iweze kuendelea kushika dola na kuwaletea amani na maendeleo wananchi wake.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.