TAKUKURU yaagizwa kukamata wakurugenzi

MZALENDO - - MBELE - NA PETER KATULANDA, MWANZA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mwanza, imeagizwa kuwahoji na kuwakamata wakurugenzi na maofisa elimu waliokalia na kufuja fedha za uboreshaji wa miundombinu ya shule za sekondari mkoani hapa.

Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella juzi wakati akifunga kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa baada ya Ofisa Elimu wa Mkoa, Hamis Maulid, kutoa taarifa kuwa wakurugenzi na maofisa hao wamezikalia

Inatoka uk. 1

fedha.

Alisema fedha hizo zilizotolewa na serikali tangu Januari 2016, lakini baadhi bado ziko kwenye akaunti za halmashauri hizo wakati nyingine zikiwa hazijulikani zinafanya kazi gani.

Maulid alizitaja halmashsuri za Kwimba, Ilemela na Buchosa kuwa hazijatekeleza agizo la serikali na kuzitaja zilizotekeleza kuwa ni Nyamagana yenye shule moja ya Igelegele, Misungwi (sh, milioni 67.7) wana shule tatu za Iluja Mate, Shilole na Nyabumanda na Ukerewe shule tano (sh. milioni 702) huku Magu yenye shule tatu (sh. milioni 320.4) ikisuasua.

ìKwimba ina shule ilipewa sh. milioni 532.8, Buchosa shule mbili za Lughata na Maisome sh. milioni 411.

ìNakuagiza kamanda wa TAKUKURU mkoa kuwahoji na kuwakamata wahusika watakaobainika kufuja fedha hizo, fuatilia na kufikia Alhamisi ijayo utoe taarifa ya fedha hizo zilipo,î aliagiza Mongella na kudai wakati wa kuchekeana umepita.

Mkuu huyo wa mkoa alisema ofisi yake inazo taarifa kuwa idadi ya watoto wa darasa la 1-7 inayotolewa na baadhi ya shule za msingi si sahihi, imeongezwa kwa ajili ya ulaji na kutolea mfano kuwa shule moja ina watoto 500, lakini wameambiwa wapo 700.

ìIjuma ijayo naomba nipate taarifa ya idadi halisi ya wanafunzi kutoka katika shule zote za msingi, baadhi ya walimu wanakula fedha wanazopelekewa na kudai wapo wanafunzi 700 wakati ni 500,î alisema na pia kuwaonya maofisa wa TASAF wanaojihusisha na ulaji wa fedha za kaya masikini waaache mara moja.

Mongella aliwaomba vongozi wa vyama vya siasa, wabunge, madiwani, wenyeviti wa Halmashauri za wilaya zote mkoani hapa waachane na siasa uchwara na kushirikiana na serikali kusukuma maenddeleo ya wananchi mbele.

MAKAMU wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB ) Dk. Frannie Leutier, akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kulia) namna ya kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo, Dar es Salaa,jana.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.