Nape atuma salamu za rambirambi

MZALENDO - - MAKALA - NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Joseph Senga na wanahabari wote nchini, kufuatia kifo cha aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima na mwanahabari mkongwe Joseph Senga

Senga alifariki dunia Julai 27 mwaka huu nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.

Katika salamu zake Nape amesema tasnia ya habari imempoteza mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya tasnia ya habari nchini.

“Joseph Senga alikuwa mwanahabari shupavu na hodari, ambaye siku zote alisimama kidete kupigania maendeleo ya tasnia ya habari na kutenda haki katika tasnia hiyo.

“Napenda kutoa salamu zangu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu”

Nape pia amewaombea wote walioguswa na kifo cha Senga kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki cha kuondokewa na mpendwa wao.

RAHA YA MILELE UMPE EEEH... BWANA, NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE APUMZIKE KWA AMANI AMINA.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.