Spika Ndugai aagiza kamati za Bunge kukutana Dodoma

MZALENDO - - MBELE - NA JACQUELINE MASSANO

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai ameagiza mikutano yote ya Kamati za Kudumu za Bunge inayotarajia kuanza Agosti, 22 mwaka huu kufanyikia mjini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ni kwamba, maagizo hayo ya Spika ni utaratibu endelevu kwa vikao vingine vya Kamati za Bunge vitakavyofuatia.

ìMaagizo ameyatoa katika waraka wake Na. 6/2016 kwa waheshimiwa kwa kuzingatia Kanuni ya 117(4) ya kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la Januari, 2016 inayosema: ìMikutano ya kawaida ya Kamati za Kudumu itafanyika Dodoma, Dar es Salaam au Zanzibar.î

ìKwa kuzingatia maagizo ya serikali kuchagiza uhamiaji wa Makao Makuu mjini Dodoma kwa mawaziri na watendajiwa serikali ambao kimsingi ndiyo wahusika wakuu wanaokutana na Kamati za Kudumu za Bunge,îilisema taarifa iliyo.

Katika waraka wake huo, Spika Ndugai alisema Bunge ni mhimili ambao tayari ulikwishatekeleza kwa vitendo kuhamia Dodoma kwa baadhi ya mikutano yake kufanyika Makao Makuu tangu Oktoba, 1974.

ìNa baada ya uchaguzi Mkuu mwaka 1995, mikutano yote ya Bunge ilihamishiwa Dodoma.

ìHata hivyo, vikao vya kamati ambavyo hufanyika kabla ya mikutano ya Bunge viliendelea kufanyika Dar es Salaam kwa kuwa vilihitaji uratibu wa karibu wa serikali ambayo ilikuwa ikiendesha shughuli zake Dar es Salaam.î

Ndugai alisema kwa kuwa mhimili wa Bunge umeshahamia Dodoma na baadhi ya huduma za utawala na watumishi waliendelea kuwa Dar es Salaam kwa mawasiliano ya karibu na serikali, kwa sasa nao watahamia makao makuu.

Aliongeza kuwa hivi sasa Bunge na serikali vinaelekea kuwa mahali pamoja kwa sababu mji ambao Bunge linakutana ndiyo hapo yanapokuwa makao makuu ya serikali.

ìHuku mbele kutafanyika tathmini iwapo mfumo wa sasa uliopo wa mikutano ya Bunge kutanguliwa na vikao vya kamati na Bunge kwa pamoja kama ilivyo kwa nchi nyingine katika mifumo yao ya Bunge pale ambapo Bunge na Serikali wapo katika mji mmoja,î alifafanua Ndugai.

Aidha, laisema kufuatia maagizo hayo, wabunge na watendaji katika vikao vya kamati wanatakiwa kujipanga kukutana Dodoma kwa kuzingatia ratiba za kila kamati zitakazotolewa hapo baadaye.

Mkutano wa nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajiwa kuanza Septemba 6, mwaka huu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.