Dk. Shein kufungua mkutano Diaspora

MZALENDO - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, anatarajia kufungua mkutano wa tatu wa Watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) utakaofanyika kwa siku mbili mjini Unguja.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika kuanzia Agosti 24, mwaka huu hadi Agosti 25,mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Salum Maulid Salum, ilisema mkutano huo unatarajiwa kufungwa na Rais Dk. John Magufuli.

Salum alisema mkutano huo wenye kauli mbiu ya ëBridging Tanzania Tourism and Investmentí unatarajiwa kuwashirikisha wana diaspora 450.

Alisema mkutano huo una lengo la kuwahamasisha wana diaspora kushiriki katika kuendeleza sekta ya utalii ikiwa ni njia mojawapo ya kukuza uwekezaji nchini.

ìKatika mkutano wa mwaka huu kama ilivyokuwa kwa miaka iliyopita, washiriki watapata fursa ya kubadilishana mawazo juu ya mbinu na mikakati kuimarisha mazingira yatakayowezesha wana diaspora kuongeza kasi ya ushiriki wao katika kuijenga Tanzania, ikiwemo kutambua fursa zaidi za uwekezaji ulingana na uwezo, uzoefu na taaluma walizonazo kwa kushirikiana na Watanzania waliopo nchini,îalisema.

Katibu Mkuu huyo alisema kwa miaka mitatu mfululizo, serikali kwa kushirikiana na jumuia za Watanzania wanaoishi nchi za nje, imekuwa ikiandaa mikutano ya aina hiyo ambayo imekuwa jukwaa muhimu la mawasiliano na mashauriano kati ya wadau na wana diaspora juu ya namna bora ya ushirikiano kati yao.

Mkutano huo ambao unaandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, utafanyika kwa mara ya kwanza Zanzibar kutokana na mikutano miwili ilifanyika Dar es Salaam.

Mkutano wa kwanza ulifanyika mwaka 2014 na kauli mbiu ilikuwa “Connect, Engage, Inform and Envestí wakati ule wa mwaka jana ulibeba kauli mbiu ya ëCreating, Linkages between Diaspora na Local SMEs ina Tanzania”.

MHANDISI wa Mahakama ya Tanzania, Khamadu Kitunzi akimuonyesha ramani ya jengo la Mahakama ya Mwanzo Kigamboni, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Ferdinand Wambali wakati akikagua ujenzi wa jengo hilo, Dar es Salaam, jana.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.