Vigogo watano Nzega wasimamishwa kazi

MZALENDO - - HABARI - NA ALLAN NTANA, NZEGA

WATUMISHI watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, wamefukuzwa kazi na wengine wawili wameshushwa vyeo kwa tuhuma za kutafuna sh. milioni 190 za Mfuko wa Afya ya Jamii (CFH) na za chanjo.

Kufukuzwa kazi kwa watumishi hao kunafuatia uamuzi uliotolewa na Baraza la Madiwani wilayani hiyo baada ya kuridhishwa na uchunguzi uliofanywa na kubainika walitafuna kiasi hicho cha fedha.

Waliofukuzwa kazi ni Mweka Hazina, Stanslaus Lawrence, Katibu wa Afya wilaya, Kisusi Sikalwanda, Mratibu wa Chanjo, Joel Mjondora , Ofisa Ugavi Selemani Charahani na Mtendaji wa Kijiji, Said Madua .

Pia, walioshushwa vyeo ni aliyekuwa daktari wa wilaya hiyo, Emmanuel Mihayo na Mhasibu wa halmashauri ya wilaya hiyo, Denis Gombeye.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Marco Kiwele, alisema watumishi hao walishindwa kuwajibikaipasavyokatikanafasi zao na kufanya udanganyifu na uzembe ulioisababishia hasara halmashauri hiyo.

Kiwele alisema watumishi waliofukuzwa kazi kutokana na ubadhirifu watafikishwa katika mkono wa sheria kutokana na makosa waliyoyafanya.

Alisema kila mtumishi hatapata haki yake kulingana na makosa aliyofanya wakati akiwa mtumishi wa halmashauri hiyo.

Mwenyekiti huyo aliwataka watumishi kuhakikisha wanawajibika ipasavyo na kuwa bila kufanya hivyo hakuna mtu atakayewavumilia na wao wanaofanya kazi kwa mazoea mwisho wao umefika.

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi kutoka kwa kinamama wa Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni wakati wa kilele cha sherehe za Siku ya Kizimkazi, Zanzibar, juzi. Wa pili kushoto ni Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi ambae pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, ,Katiba,Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.