Bomoa bomoa yakumba vigogo

Wamo makada wa CCM, madiwani na wafanyabiashara

MZALENDO - - MBELE - NA SAMSON CHACHA, TARIME

NYUMBA zaidi ya 30 zikiwemo za ghorofa na kituo cha mafuta vimebomolewa kutokana na kujengwa ndani ya hifadhi ya barabara katika mji wa Sirari wilayani Tarime mkoani Mara.

Kazi ya uvunjaji ilianza jana asubuhi katika barabara kuu na kuongozwa maofisa wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) huku kukiwa na umati

mkubwa wa wananchi wakishuhudia majengo hayo yakivunjwa yakiwemo ya wafanyabiashara Daud Sereria aliyevunjiwa jengo la ghorofa.

Nyingine iliyovunjwa ni kituo cha mafuta cha mfanyabiashara biashara maarufu na kada wa CCM, Peter Zakaria, baa na nyumba ya kulala ya mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa wa CCM, Laurent Nyablangeti, jengo la Diwani wa Kata ya Gwitiryo, CCM, Adam Nyawambura na jengo la aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa Kata ya Sirari, Amos Sagara na majengo mengineyo.

Meneja wa TANROAD Mkoa wa Mara, Mhandisi Emmanuel Korroso, alisema wameamua kuvunja nyumba hizo zikiwemo za watu waliokua wamefungua kesi na kuzuia kuvunjiwa nyumba zao kwa muda mrefu na kesi hizo zimetolewa uamuzi ambapo wadai walishindwa.

ìWalijenga majengo katika hifadhi ya barabara ndani ya mita 23 na tulishawapa notisi ya kuondoa majengo yao kwa mda mrefu ambapo baadhi walitikia na kuondoa na wengine kukaidi agizoÖ tumeamua kuvunja majengo hayo kwa mujibu wa Sheria,” alisema Korroso. Baadhi ya waliovunjiwa walipohojiwa walisema watumishi wa TANROADS wamevunja nyumba zao na kuingia maeneo mengine ambayo hayakuwemo kwenye orodha ya kuvunjwa.

Diwani Nyawambura alisema nyumba zingine kama yake ilikuwa ivunjwe chumba kimoja na kenopi, lakini imebomolewa vyumba viwili na kenopi.

Kwa upande wake, Zakaria alisema katika chake cha kuuza mafuta nguzo mbili ndizo zilikuwa ndani ya hifadhi, lakini kituo kizima kimebomolewa.

ìWamenibomolea kituo kizima hii ni hasara ambayo wametuingizia wanatakiwa kufuata mwisho wa alama zao badala ya kuvuka alama na kuharibu mali za watu,” alisema kada huyo bila kutaja hatua watakazochukua.

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.