CHADEMA inapaswa kutii maagizo ya Tume ya Haki za Binadamu

MZALENDO - - HABARI - NA EMMANUEL MOHAMED

NENO kushughulikia ni amri ya jeshi ya kuangalia upande wa kulia, kwenda hatua moja mbele na kisha kurudi nyuma kwa kupigapiga miguu ili kurudi katika mstari na kuhakikisha kuwa mstari umenyoka sawasawa wakati wa mafunzo ya gwaride.

Kwa maneno mengine ni jambo ambalo linamfanya mtu atumie nguvu,juhudi na akili yake ili kulitekeleza kazi yake.

Baada ya kufafanua maana ya dhana kamili ya muktadha wa neno la kushughulikia imeniradhimu kuandika hoja hii kutokana na hivi karibuni Tume ya Haki za Binadamu Utawala Bora (THBUB) kutoa tamko ambalo ilililaumu Jeshi la polisi katika baadhi ya matamko yake.

Kwa mujibu wa tume hiyo, ilililaumu jeshi hilo kwa kutoa matamko mbalimbali likiwemo lile lililosomeka: “Tutawashughulikia watakaokiuka amri”.

Tume hiyo iliandaa mkutano kwa madai ya kutafuta ufumbuzi wa hali ya kisiasa nchini huku Mwenyekiti wa Tume hiyo, Bahame Nyanduga akidai matamko hayo yamekuwa yakitolewa na vyombo vya dola na yanaleta hofu ya kuchochea kwa uvunjifu wa amani na haki za binadamu.

Katika taarifa hiyo, Nyandunga alinukuliwa akidaiwa kusema “Baada ya tamko la Chadema la kufanya maandamano nchi nzima kumekuwa na matamko kutoka kwa viongozi wa kitaifa baadhi ya wakuu wa mikoa makamanda wa polisi kukataza kufanyika kwa maandamano hayo na kwamba watakaokiuka zuio hilo watashughulikiwa.”

Katika hoja yake hiyo, mwenyekiti huyo alidai tamko la polisi la kusema kuwa watashughulikiwa ni moja ya uchochezi wa uvunjifu wa amani nchini.

Hata hivyo kwa mujibu wa maandiko mbalimbali kama vile Kamusi Sanifu ya Kiswahili, imetoa maana sahihi ya neno kushughulikia hivyo si kweli neno hilo limekubaliwa kutumika kama sehemu ya amri ya jeshi hilo katika kutekeleza majukumu ya kazi zao.

Kwa undani wa maana halisi ya neno hilo ambalo Mwenyekiti wa Tume hiyo amelieleza katika dhana ya kisiasa zaidi na kwamba lionaonesha ni hali ya kuwa katika harakati ya kutekeleza jambo fulani la kimajukumu ya kikazi yaani kwenda huku na huku bila ya kutulia katika kukamilisha sehemu ya kazi.

Lakini kosa ni kutulia bila ya kukamilisha jukumu lake hivyo ni lazima askari hakikishe anafanya juhudi mbalimbali za kufanikisha jukumu lao imladi atimize maana ya neno kushughulika.

Ni hali isiyopingika kuona kuwa vyombo vya dola vinajitegemea bila ya kuingiliwa na kushawishiwa na chama cha siasa wala taasisi yeyote katika utendaji kazi wake hivyo kitendo cha Tume hiyo kuitaka jeshi la polisi kuacha matumizi ya maneno kama vile “tutawashughulikia wote watakaokaidi amri” na kudai kuwa kauli hiyo inachochea hofu ya kuvunjika kwa amani nchini.

Katika mazingira ya sasa ya kisiasa ilioko nchini kuna haja ya jeshi la polisi kuliacha kutekeleza majukumu yake ya kulinda amani hivyo hakuna wasiwasi wowote kuwa endapo jeshi la polisi likitumia kauli ya tamko la maneno hayo yataonesha viashiria vya machafuko na uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu.

Hoja yangu kubwa ni kuwa watanzania waelewe na kutambua kuwa maneno yanayotumika katika jeshi la polisi yameidhinishwa kuwa halali katika matumizi ya majukumu yao ikiwemo maneno kama vile songa mbele,usawa wa kati,tisha,kushurutisha pamoja na shambulia yanatumika kihalali kabisa.

Kuna msemo wa waswahili unasema kuwa makali ya mkuki ni ncha na si mpini wake hivyo amri za kiaskari si ncha ambayo kusema kuwa itachochea uvunjifu wa amani.

Kinachopaswa kufanyika ni kuonya taasisi,Tume na wadau mbalimbali kuacha kutumika na vyama vya siasa kuchafua taswira ya jeshi la polisi katika kutekeleza majukumu yao kama vile kulinganisha matamko ya kiamri ambayo yapo kihalali na kudai kuwa ni uchochezi wa uvunjifu wa amani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.