Ni wakati wa wanawake nchini kuchangamkia fursa za kiuchumi

MZALENDO - - HABARI -

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewahakikishia wahandisi wanawake kuwa serikali itatoa zabuni za miradi ya ujenzi kwa wahandisi wa ndani hususani wanawake kwa kuwa ni waadilifu.

Amesisitiza kuwa ni nadra kukuta wahandisi wanawake wakifuja fedha katika miradi ya maendeleo, hivyo ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara na reli nchini itakuwa bora na ya kiwango cha juu.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa wakati mwafaka kwa wahandisi wanawake kuchangamkia fursa hiyo kwa kuhakikisha zabuni watakazopata wanazitendea haki kwa kujenga kwa kiwango cha juu.

Tunaamini hilo litazidisha uadilifu waliokuwa nao kwa kufanya kazi nyingi zaidi kwa ueledi mkubwa, kwa kuwa kufuata misingi ya taaluma zao na kuhakikisha wanakuwa sehemu ya kuijenga vyema Tanzania kupitia zabuni watakazopata au watakazopewa na serikali.

Ikumbukwe kuwa miongoni mwa maeneo yenye kazi nyingi na kubwa kwa upande wa wahandisi ni serikalini, hivyo kwa wataalam hao kujipanga vilivyo kutawawezesha kuleta mabadiliko makubwa kwa taifa na kwao binafsi.

Taaluma ya uhandisi ni taaluma bora katika kuelekea maendeleo ya haraka, hivyo huu ni wakati wahandisi wa kike nchini kufanya kila liwezalo kuhakikisha wanatimiza kiu ya Makamu wa Rais Samia kwa kufanya kazi kwa ueledi mkubwa.

Kupata nafasi za kutosha kwa wahandisi, kumetokana na kuaminiwa hivyo wanapaswa kuonyesha imani hiyo, kwa kuwa wanawake ndio kila kitu, ni watu waaminifu na waadilifu kwa jambo lolote wanalokabiliana nalo.

Serikali tayari ilishasema itatoa kazi za miradi kwa wahandisi wazawa na kutoa kipaumbele kwa wahandisi wanawake ili kuongeza ujuzi na kufanya miradi hiyo kuwa salama na bora kwa kuzingatia uzalendo.

Tunaamini huu ni wakati mzuri kwa wahandisi wanawake kuzijengea uwezo kampuni zao ili ziweze kufanya kazi zao kwa umakini mkubwa pindi watakapo pata zabuni mbalimbali serikalini ili wawe na uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa bidii kubwa.

Kuwezekana kwa mambo hayo, kutazidisha uwezo na maarifa kwa wahandisi wanawake ambao wengi wanakuwa waoga katika kufanya kazi zao kwa ueledi mkubwa kwa kuwa wanaamini hawana uwezo wa kufanya vizuri kama walivyo wahandisi wa kiume.

Kila mmoja anauwezo wa kufanya vizuri ili mradi awe na nia na dhamira ya dhati, hivyo tunaamini sapoti ya serikali kwa wahandisi wanawake itachochea wanawake wengi kusoma masomo ya sayansi ili taifa liwe na wahandisi wengi wa kike.

Hivyo, tunaamini kuwezekana kwa kuwainua wahandisi wanawake kwa kuwapa zabuni ni wakati mwingine kwa kila mhandisi kufanya kazi zake kwa weeledi mkubwa ili kusaidia zabuni wanazopata zinatekelezwa kwa cha uadilifu mkubwa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.