MWAFRIKA ALIYEIDUWAZA ULAYA

Mwafrika aliyeiduwaza Ulaya

MZALENDO - - MAKALA - YAOUNDE, CAMEROON

AFRIKA ni moja ya mabara yanayotoa wachezaji wengi nyota wa soka ulimwenguni wenye uwezo mkubwa wa kusakata soka bila wasiwasi wowote.

Achilia mbali kile kizazi cha kina Didier Drogba,Nwanko Kanu,Khalilou Fadiga,Djbrie Cise,Yakubu Ayejben,Jayjay Okocha na Samuel Etoo ambao waliwika kwenye timu zao za klabu pasipo na faida ya kuzifikisha mbali timu za taifa kwenye mashindano ya kombe la Dunia na michuano ya Olimpiki.

Hata hivyo usidhani kuwa kizazi hiki cha Sadio Mane,Victor Wanyama,Alex Iwobi, Riyadh Mahrez na Mbwana Sama a ambao wanatesa kwenye klabu zao kila kukicha kuwa wataweza kuirudisha ile hadhi ya mpira wa Afrika.

Kabla ya kizazi kile cha George Weah kuieleza dunia kuwa waafrika tunaweza kufanya mapinduzi kwenye soka wakati akiwa anatwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Ballon d’Or) mwaka 1995 kipindi akiitumikia AC Milan ya Italia, kuna kizazi cha waafrika ambacho hakitasahaulika kwenye akili za wadau wa soka ulimwenguni.

Hivi umewahi kumsikia au kumuona mfalme wa soka la Cameroon na Afrika kwa ujumla aliyewaduwaza wanasoka na mashabiki kutoka Ulaya?

Sio Samuel Etoo,Thomas Makanaky wala Patrick Mboma ambao waliweza kupeperusha bendera ya Cameroon ndani ya Afrika tu.

Mfalme huyo ni mkongwe wa soka Roger Milla,ambaye aliweza kusafisha njia kwa waafrika kuthaminika kisoka katika bara la Ulaya kutokana na kile alichokifanya kwenye fainali za kombe la Dunia mwaka 1990 na 1994.

Katika makala haya tuangalie mambo mbalimbali aliyoyafanya mkongwe huyo na kulitangaza bara la Afrika kupitia mchezo wa soka.

MILLA VS KOMBE LA DUNIA 1990

Baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika(AFCON) mwaka 1988,timu ya taifa ya Cameroon ilikwenda kushiriki kombe la Dunia mwaka 1990 nchini Italia huku ikiwa na nyota kama Thomas Makanaky,Steven Kunde na mkongwe Milla.

Ambapo Cameroon walipangwa kundi B huku wakiwa na timu kama Argentina,Umoja wa nchi za Soviet na Romania, kwenye mchezo wao wa kwanza uliopigwa uwanja wa Milan Juni 8 mwaka huo.

Katika mchezo huo, Cameroon iliichapa Argentina kwa bao 1-0 bao lililofungwa na Fracos Biyick lakini Milla hakuonyesha kiwango kikubwa kutokana na kuingia uwanjani akitokea benchi dakika ya 81.

Kwenye mchezo wa pili ambao walicheza na Romania, Roger Milla akaudhihirishia umma na wadau wa soka ulimwenguni kuwa yeye ni nani baada ya kuifunga Romania mabao 2-0 wakati alipotokuwa ametokea benchi dakika ya 61, huku Cameroon ikiibua vinara wa kundi hilo chini ya Romania na kufuzu hatua ya mtoano.

Mnamo Juni 23 mwaka huo Roger Milla aliendelea kuuduwaza umma wa wanandinga ulimwenguni baada ya kuingia kwenye dakika ya 54 ya mchezo na kufunga mabao mawili huku akiitengenezea rekodi Cameroon kuwa ndio timu ya kwanza Afrika kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Milla aliendelea kufanya vizuri kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya England ambapo alitokea benchi na mpira wake wa kwanza kuugusa alisababisha penalti ambayo iliweza kufungwa Emanuel Kunde na baadaye alitoa pasi ya mwisho ya bao lililowekwa kimiani na Eugene Ekeke lakini kwa bahati mbaya Cameroon waliweza kutolewa kwa kufungwa mabao 3-2. MILLA VS KOMBE LA DUNIA 1994 Licha ya Cameroon kutolewa kwenye hatua ya makundi kombe la Dunia mwaka 1994, Roger Milla aliweza kutengeneza rekodi ya kuwa mchezaji pekee mwenye umri mkubwa kufunga bao kwenye kombe la Dunia ambapo alikuwa na umri wa miaka 42.

WASIFU WAKE KAMILI

Anaitwa Albert Roger Mooh Miller maarufu kama Roger Milla alizaliwa Mei 20 1952, Younde nchini Cameroon.

Alistaafu kucheza mpira akiwa na umri wa miaka 42 baada ya kuitumikia timu ya taifa ya Cameroon kwa zaidi ya miongo miwili akicheza nafasi ya mshambuliaji.

Ni mmoja kati ya nyota wa Afrika wasiosahaulika kwenye medani ya soka kwa mafanikio aliyoyapata kutokana na juhudi zake alizozionyesha.

Aliweza kucheza fainali tatu za kombe kwenye mwaka 1986,1990 na 1994 akiwa na Cameroon.

Atakumbukwa sana kwa ile aina yake ya ushangiliaji wa goli kipindi anapofunga anakimbia hadi kwenye bendera ya kona na kuanza kucheza dansi.

MAISHA YAKE KISOKA Alianza kucheza mchezo wa soka kwenye klabu ya Leopards Douala mwaka 1970-1974 bila ya malipo ya ain yeyote.

Aliweza kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ndani ya Afrika akiwa na umri wa miaka 18 mwaka 1976 akiwa na klabu ya Tonnere Younde.

Mwaka 1977 alianza kucheza soka l kulipwa nchini Ufaransa kwenye Klabu ya Valenciennes.

Baada ya timu hiyo Milla aliweza kuzitumikia timu kama Bastia,AS Monica,Saint Etiene na Montpeleire.

Huku akitwaa mataji mbalimbali nchini Ufaransa pamoja na kombe la Ufaransa mwaka 1980 na 1981. Milla aliweza kucheza mechi 63 na kufunga mabao 37 kwenye michezo ya kimataif akiwa na Cameroon.

Alitwaa Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 1975.

TUZO BINAFSI

Milla aliweza kutwaa tuzo ya mchezaj bora wa Afrika mwaka 1976 na 1990.

Pia mwaka 1986 Milla aliweza kutwa tuzo ya mchezaji bora wa AFCON.

Mwaka 1986 na 1988 aliweza kutwa tuzo ya mfungaji bora wa Afrika.

Alitwaa tuzo ya mfungaji bora wa kombe la Dunia mwaka 1990 akifunga mabao 6 na akaorodheshwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu bora ya duni mwaka huo.

Hata hivyo Milla ndiye mchezaji peke wa Afrika kuimiliki tuzo ya mwanasok bora Afrika kwa kipindi chote.

Imetayarishwa na Abdul Dunia (TSJ) kwa msaada wa mitandao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.