Dc Hapi azindua mafunzo ya ujasiriamali Kinondoni

MZALENDO - - MATANGAZO/HABARI - NA CHRISTOPHER LISSA

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi (pichani),amezindua mafunzo ya wajasriamali wilayani hhauymoowahyuaktiulie amkiawanataankiailimwaafwunezzoe kujinufaisha kiuchumi.

Uzinduzi huo, uliofanyika katika viwanja vya TTCL, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam, uliambatana na maonyesho ya bidhaa zilizotengenezwa na vikundi vya ujasiriamali wilayani humo.

Akizindua mafunzo hayo, Hapi alisema, mbali na kulenga kutoa stadi za ujasiriamali, pia yanakusudia uhamisishaji wa wananchi kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa.

“Tumefanya usajili wa vijana zaidi ya 10,000 kutoka mitaa ya Kinondoni, ambao wameonyesha nia ya dhati ya kupata mafunzo hayo,”alieleza Hapi.

Alisema mafunzo hayo yatatolewa bure kwa vikundi vyote ambapo katika hatua ya awali itakuwa ni kutoa elimu na stadi za ujasiriamali, namna ya kuanzisha , kusimamia na kuendeleza biashara na mbinu katika uendeshaji shughuli za ujasiriamali.

“Nia ni kubadilisha fikra za watu, badala ya kukaa vijiweni, kuzunguka na wasifu zao, wabuni njia nyingine za kujiingizia vipato,”alisema Hapi.

Aliongeza kuwa serikali iko tayari kuwasaidia kwa kuwaonyesha fursa za mikopo, kuboresha biashara zao ili sasa wtuewnegziezaikduiwkaatiknaanchiwyaejtaus”iriamali

Alisema hali hiyo itasaidia kuwaingiza wajasiriamali hao katika mfumo rasmi, ili waweze kupata manufaa makubwa zaidi na kujenga uchumi wao, kuliko sasa.

“Lengo ni kutekeleza diya ya taifa ya kutengeneza taifa lenye viwanda. Huwezi kutengeneza taifa lenye viwanda kama watu wote wanasubiri kuajiriwa tu. Umefika wakati sasa wa kuachana na mfumo huo,” alisema mkuu huyo wa wilaya.

Aliongeza kuwa: “Hatuwezi kulifikisha taifa katika uchumi wa kati kama hakuna watu wanaojishughulisha katika kilimo na ujasiriamali.”

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.