Facebook ndio mtandao pekee wenye watumiaji zaidi ya bilioni 1

MZALENDO - - JILIWAZE -

BILA shaka unahusika na matumizi ya mitandao ya kijamii,kama si yote ifahamikayo basi ni moja au miwili utakuwa unatumia. Hapa namaanisha mitandao ya kijamii ya facebook,twitter na mingineyo unayoijua kwa sababu siku hizi ni mingi kama mchanga wa baharini.

Facebook ukiwa ni miongoni mwa mtandao wa kwanza wa kijamii unamilikiwa na mmarekani Mark Elliot Zuckerberg ulianzishwa rasmi mwaka 2003.

Tokea wakati huo mtandao huu umekuwa ukiwaunganisha watu tofauti tofauti kutoka nchi mbalimbali duniani.

Vijana kwa wazee,wakinababa na kinamama,watoto kwa wakubwa wamekuwawakitumia muda wao wa ziaada kuperuzi na kufanya soga katika mtandao huu.

Pamoja na hivi sasa duniani kushuhudiwa mlipuko wa mitandao hii huku mingine ikiwa haina umaarufu wowote lakini bado Facebook inaonyesha kuwa bado ipo kangangari na inakubalika na watu.

Kuna wakati Serikali ya China iliupiga marufuku mtandao huu usifanye kazi nchini mwake, sababu mbalimbali zilitolewa ikiwemo sababu ya lugha amabyo ilikuwa ni kiingereza.

Mr Zuckerberg ikambidi alifanyie kazi sula hilo kwani kwa namna moja au nyingine ingeweza kumpunguzia faida aliyokuwa akipata kutoka katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi duniani.

Tokea wakati huo facebook imeendelea kufanya kazi na kuwa na watu wengi zaidi nchini China.

Lakini JE WAJUA kuwa Facebook inawatumijai sawa na raia wa taifa hilo kubwa katika bara la Asia?

Ndiyo takwimu zilizotolewa hivi karibuni zimebainisha kuwa mtandao wa Facebook unakaribu watumijai bilioni 1.3 ulimwenguni kote sawa na China yenye wakazi bilioni 1.3.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.