Mlo wa mpangilio ni bora kwa afya yako

MZALENDO - - JILIWAZE - NA MWANDISHI WETU

ILI kuwa na siha njema ni muhimu kula vizuri. Kula vizuri si rahisi, ingawa wengi wetu tunadhani kula vizuri ni kula chakula tunachokipenda ñ chips, kuku, mayai, nyama na vingine. Hii ni kasumba mbovu tu. Kula vizuri (au balanced diet) si lazima kula vyakula unavyopenda, bali kula vyakula vyenye afya na kujenga mwili wako.

Njia moja mbadala ya kuhakikiasha unakula vizuri na kwa afya ni kuwa na ratiba ya wiki ya chakula. Leo tunaangalia umuhimu wa kupanga ratiba ya chakula kwa afya yako na familia yako.

Chakula bora (Balanced diet) ni chakula kinachokupa virutubisho vyote muhimu mwilini katika milo mitatu ya siku.

Chakula bora, kama ilivyo kwa kila kitu bora, hakiliwi kwa bahati, bali huhitaji mipango madhubuti ya kupanga chakula cha kila siku kinachojali afya yako na familia.

Sasa, kuandaa ratiba ya chakula kizuri si kazi rahisi, lakini inasaidia kupunguza mawazo ya nini cha kupika na kupunguza haraka za kuandaa vyakula bila kufikiria vizuri virutubisho vinavyopatikana kwenye milo yako. Kwa kawaida ni kazi ya mama kuamua chakula gani kinaliwa nyumbani.

Lakini, mie nadhani ni swala la familia nzima kuamua chakula gani kinafaa kuliwa sababu chakula ni swala la kila mtu kwenye familia. Hapa ndio panapotuleta kwenye swala zima la kupanga ratiba ya chakula kwa wiki nzima.

Chakula ni kitu muhimu sana maishani, hivyo ni jukumu la kila mtu kuchangia mawazo kwenye afya ya familia, si jukumu la kumuachia mama pekee - kila mtu ana nafasi yake kwenye kutoa mchango, hata kama ni wa mawazo.

Kama uko peke yako usikate tamaa, ni rahisi zaidi maana utakuwa una uwezo wa kufanya maamuzi bila kuwa na mawazo ya kukinzana.

Sual la kuamua chakula gani kinaliwa lini ni swala la mipango na malengo. Ukifanya hivi unaweza kujijengea ratiba ya kula milo vizuri iliyojaa virutubisho unavyohitaji. Na jambo kubwa hapa ni kuokoa muda na matumizi yasiyo na tija.

Itaendelea

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.