Baraza la Madiwani lampa maagizo Ofisa Elimu

MZALENDO - - HABARI - NA PRISCA MSHUMBUSI, UKEREWE.

BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, limemtaka Ofisa Elimu msingi, Reginald Richard, kurudisha madawati aliyoyatoa kimakosa katika shule sita na badala yake yapelekwe katika shule mbili husika.

Akitoa agizo hilo jana katika kikao cha madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, George Nyamaha alisema madawati hayo yalitolewa kimakosa na kufanya baadhi ya watu kulalamika.

Nyamaha alisema mfadhili kutoka kampuni ya Tigo alitoa madawati 200 kwa ajili ya shule za msingi Bukongo na Mwitongo.

ìNashangaa kuona maagizo yanageuzwa na watu kwa manufaa yao, ni bora kufanya kitu kilicho sahihi ili kuweza kwenda na wakati, lakini inapofikia muda tunageuza jambo kinyume hatutaeleweka kwa hao wanaojitolea kusaidia watoto wetu kuweza kusoma kwa bidii,î alisema Nyamaha.

Diwani wa Kata ya Igalla, Joshua Bituro (CCM), alifafanua kuwa Tigo ilitoa madawati kwa ajili ya kugawa lakini Ofisa huyo aliyagawa kinyemela pasipo kuwashirikisha madiwani na uongozi wa halmashauri.

ìUjue unapofanya kitu ni bora kumshirikisha mtu kwani Ofisa huyu hana faida yoyote kwa sababu ameweza kugawa madawati kinyemela na wafadhili wakiona hivyo wanaweza kuacha kusaidia, kutokana na kukengeuka na maagizo yao,î alisema Bituro.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Pelagia Sogoti, alisema kabla ya kwenda kutoa madawati hayo wataweza kukaa na walimu na wanafunzi ili wawaeleze juu ya kutolewa kwa madawati hayo na kuwaondolea hofu wanafunzi kwani tayari wameshayatumia.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.