Lipumba amtia kiwewe Mbowe

MZALENDO - - MBELE - NA EMMANUEL MOHAMED

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akimkaribisha Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD cha Burundi, Evariste Ndayishimiye, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, jana. Kushoto ni Mnadhimu Mkuu wa CNDD-FDD, Gelase Ndabirabe. (Picha na Bashir Nkoromo).

KUREJEA kwa kishindo kwa Profesa Ibrahim Lipumba katika nafasi ya uenyekiti wa CUF, kumemtia kiwewe Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ambaye sasa amewapiga mkwara viongozi wa UKAWA wanaomuunga mkono Lipumba huku akiwatishia kuwatimua uanachama.

Profesa Lipumba alirejea kwenye kiti hicho, baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kupitia barua yake yenye kumbukumbu HA.322/362/14/85 iliyohusu ushauri wake juu ya mgogoro wa CUF, kusema Profesa Lipumba bado ni kiongozi wa chama hicho.

Alisema baada ya kupitia katiba ya CUF alibaini kuwa Lipumba bado ni mwenyekiti wa taifa halali wa chama hicho.

Mbali na Lipumba, Msajili pia alisema viongozi na wanachama wote wa CUF waliosimamishwa na kufukuzwa uanachama bado ni wanachama halali kwa kuwa vikao vilivyotumika kuwaondoa vilikuwa na kasoro za kisheria.

Kwa mujibu wa Mbowe endapo atabainika kiongozi ama mwanachama wa chama chochote kinachounda UKAWA kusikiliza maneno ya Lipumba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa na pamoja na kufutiwa uanachama wa chama husika.

Mbowe alisema kiongozi ama mwanachama wa UKAWA atakayekuwa karibu na Lipumba atavuliwa uanachama mara moja.

Aidha alisema UKAWA haimtambui nafasi yake ya Uenyekiti wa CUF na wala uanachama wake hivyo hatambuliki ndani ya UKAWA na kuwataka wafuasi wa chama hivyo kutomfuata.

ìWanasheria na mawakili wa UKAWA wanatakiwa kuhakikisha maslahi ya vyama vyote vya UKAWA yanalindwa na endapo atatokea mwanachama anayetaka kuleta mgongano ndani ya chama ni vyema wanasheria hao wakamshughulikia harakaîalisema.

Aliongeza kuwa wanasheria na mawakili wa UKAWA wanatakiwa kuwaadhibu mara moja viongozi watakaosababisha mitafaruku na kwamba hao ndio wanaoleta mikwaruzano ndani ya UKAWA.

Mapema juzi Maalim Seif alimgwaya Profesa Lipumba baada ya kushindwa kufika ofisi za makao makuu ya CUF Buguruni kama alivyotangaza awali.

Maalim Seif alitangaza kwenda ofisini hapo kwa mara ya kwanza baada ya kurudi kwenye matibabu na ziara nje ya nchi, akisindikizwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge na madiwani wa chama hicho.

Alizungumza akiwa ofisini hapo, Profesa Lipumba, alisema anamkaribisha Maalim Seif kwa kuwa ni Katibu Mkuu wa CUF na kwamba yupo tayari kushirikiana naye kuendesha CUF.

Hata hivyo, wakati Profesa Lipumba akitoa msimamo huo, wafuasi wa chama hicho walimtaka na kumhadharisha Maalim kwamba atakapokanyaga ofisini hapo ni lazima amtambue Profesa Lipumba ni mwenyekiti wa taifa wa CUF.

Baadhi ya wafuasi wa chama hicho walisema iwapo hatafanya hivyo watamtimua.

Naye Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji, akizungumza kwa niaba ya wabunge wengine wa CUF, alisema waliahirisha kwenda ofisini hapo ili kuepusha shari.

Alisema hakuna sababu ya kuamsha ghasia kwa ajili ya ofisi hizo kwa kuwa hilo ni jengo tu lakini wao wanao uwezo wa kufanya shughuli za CUF, hata nje ya ofisi hizo na kwamba wao wanasimamia uamuzi uliotolewa na vikao halali.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.