Ramani zilizopitwa zachochea upotoshaji

MZALENDO - - HABARI - NA RACHEL KYALA

KUPITWA kwa wakati kwa ramani, kumechangia kudhoofisha huduma mbalimbali kutokana na kukosekana taarifa sahihi jambo linalochochea kutolewa uamuzi usio sahihi.

Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Justo Lyamuya, alisema hayo jijini Dar es Salaam, wakati wa warsha maalumu iliyowahusisha wadau wa masuala ya kijiografia.

ìLengo la warsha hii ni kukusanya ramani zote zilizopo nchini, kwa kuwa ramani hizo zinatofautiana, tutaona namna tunavyoweza kupata ramani moja sahihi ambayo itatumika rasmi,îalisema.

Pia, alisema mkutano huo utaandaa mfumo wa utunzaji taarifa mbalimbali za kijiografia ambapo kila mhitaji atazipata kwa kulipia, badala ya kila mtu kujitafutia mwenyewe na kupotosha usahihi.

ìTutakuwa na kipindi cha mpito cha kuweka sera ya taarifa ambapo huduma hiyo itasaidia watoa uamuzi kupata taarifa sahihi na kufanya uamuzi,îalisema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Yamungu Kayandabila, akifungua warsha hiyo, alisema serikali kuu ipo tayari kushirikiana na sekta binafsi, serikali za mitaa na wadau wengine kuhakikisha mfumo huo unafanikiwa.

ìMipaka sahihi itasaidia kuchochea ukuaji uchumi na kuboresha huduma za jamii kwenye sekta ya umma, ndio maana imetoa msukumo kufanyika kwa shughuli hii,îalisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.