Wawekezaji waitwa kuwekeza sekta ya usafiri majini

MZALENDO - - HABARI - NA SOPHIA WAKATI,TANGA

WAWEKEZAJI wa nje na ndani katika sekta ya usafiri wa majini nchini hapa wametakiwa kuwekeza na kutumia fursa za kiuchumi zilizopo ili kuweza kuleta maendeleo endelevu kwa taifa.

Hata hivyo,pia serikali imetakiwa kutoa elimu zaidi kwa watumiaji wa bahari ikiwemo matumizi ya vifaa vya uokoaji ili kuepusha majanga na vifo vya watu vitokanavyo na usafiri huo wa majini.

Kauri hiyo imetolewa jana na Waziri wa viwanda,biashara na masoko nchini Zanzibar,Balozi. Amina Ally Salum wakati wa kufunga maadhimisho ya wiki ya bahari duniani ambayo kitaifa yalifanyika mkoani Tanga.

Alisema kwamba elimu na mafunzo ya mara kwa mara ni muhimu kwa watumiaji ili kuifanya sekta hiyo ya usafirishaji majini kuwa madhuti na nguzo ya maendeleo ya taifa na dunia kwa ujumla.

ìBado kuna haja ya kuiangalia sekta ya usafiri wa majini ili kuhakikisha usalama bora kwa watumiaji,watoa huduma baharini na wananchi kujifunza zaidi kutaepusha vifoîalisema Balozi Amina.

Aidha,BaloziAmina ambaye alikuwa akimwakilisha Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na usafirishaji Zanzibar,Ally Karume ambapo pia alisema ipo haja ya serikali kuwekeza zaidi kwenye sekta hiyo ya bahari.

Alisema kuwa usafiri wa majini hauepukiki hivyo kuna haja ya kutumia mkakati shirikishi ili kujenga muelekeo wa pamoja kutimiza majukumu na kuleta ufanisi na upatikanaji bora usafiri wa majini.

Balozi Amina akizungumzia zaidi, alisema kwamba ukosefu wa vifaa vya kutosha vya uokoaji inapelekea watu wengi kupoteza maisha pindi zitokeapo ajali njia za majini.

“Watu wengi chini hawana elimu ya vyombo vya majini hivyo ni vyema elimu ikatolewa mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kuwa na vifaa vya uokoaji ambavyo vitasaidia kuokoa maisha ya watu pindi inapotokea ajali”alisemaAmina.

Waziri,Amina alitumia nafasi hiyo kwa kuwataka wazazi wa mkoa wa Tanga na tanzania kwa ujumla kuachana na mazoea na badala yake wawapeleke watoto wao katika vyuo vya ufundi kujiandaa na ujio wa bomba la mafuta.

Akizungumzia kwa upande wa mabaharia kutoka Zanzibar,Masoud Yunus alisema kuwa wapo ambao wamepata elimu ya kutosha ya mambo ya ubaharia hivyo ni vyema serikali ikawashirikisha pindi mradi huo utakapoanza.

“Tupo ambao tumepata elimu ya kutosha ya bahari hivyo ni vyema serikali ikatupa ajira na kutushirikisha pindi mradi huo utakapoanza”alisema

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.