Askari ajiua kwa risasi Iringa

MZALENDO - - HABARI - NA ANITA BOMA, IRINGA

ASKARI wa Jeshi la Polisi kituo cha Mafinga wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa, mwenye namba G 7444 PC Obed Mwaipopo ( 28 ) amekatisha maisha yake baada ya kujipiga risasi kichwani na kufariki dunia papohapo.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa ACP Julias Mjengi alisema tukio hilo lilitokea Septemba 28 mwaka huu saa moja usiku katika kituo cha Mafinga cha polisi.

Alisema akiwa na wenzie katika majukumu yake ya kazi ambapo alikuwa lindo siku hiyo katika kituo hicho akiwa na wenzake alijiua kwa kujipiga risasi aliyokuwa nao kichwani na kufariki hapo hapo.

Kamanda Mjengi alisema askari aliyokuwa kuwa nao walistukia mlio wa risasi na kumuona mwenzao akianguka chini na walipomwangalia alikuwa ameshafariki dunia.

Aidha,kamanda huyo aliwaambia waandishi wa habari sababu za kijiua kijana huyo hazijajulikana kwa sababu hakuacha ujumbe wowote ambao ungebaini sababu za yeye kukatisha uhai wake.

“Kijana huyu ni mdogo mimi kama bosi nimeingiwa na simanzi kumpoteza kwani ni kijana ambaye alikuwa mtaratibu, lakini hatuwezi kusema chochote kwa sababu hatuwezi kujua nini kilimsibu hadi kufikia kufanya uamuzi huo”alisema kamanda huyo.

Alisema marehemu hakuwa na mke wala mtoto, hivyo jeshi hilo linaendelea na uchunguzi kubaini nini kilimpelekea kuchukua uamuzi huo wa kujiua na kuwa marehemu alisafishwa juzi na amezikwa jana kijijini kwao Ipinda wilayani Kyela mkoa wa mbeya.

Hata hivyo, Kamanda huyo aliwataka vijana wake wa jeshi hilo wanapokuwa na jambo linalowasumbua moyoni mwao basi kuwashirikisha wenzao, viongozi wao wanaowamini au hata ndugu zao kwa lengo la kupata ushauri badala ya kukaa nayo moyoni.

Wakati huo huo,kichanga kinachokadiliwa kuwa na miezi saba hadi nane kimekutwa kikiwa kimefariki baada ya kutupwa na mtu asiyefahamika katika chooni cha nje cha nyumba ya Selemani Saidi mkazi wa mtaa wa msichoke kata ya makorongoni manispaa ya Iringa.

Kamanda Mjengi alisema tukio hilo lilitokea Septemba 28, mwaka huu saa 10 jioni ambapo jeshi hilo lilipata taarifa kutoka kwa ofisa mtendaji wa kata ya makorongoni kuwa katika choose cha nje cha nyumba ya mzee huyo Saidi kumeonekana kichanga hicho.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.