Chuo cha Wanyamapori chakaliwa kooni

MZALENDO - - HABARI - NA PRISCA MSHUBUSI, MWANZA

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Injinia Ramo Makani, ametoa agizo kwa Chuo cha Wanyamapori cha Pasiasi mkoani Mwanza, kukamilisha madawati 8,000 yaliobaki ifikapo Oktoba 30 na kuyakabidhi sehemu husika.

Akitoa agizo hilo jana katika uzinduzi wa shughuli ya ugawaji wa madawati waliyoahidi na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe katika bunge, kuwa Wakala wa Huduma na Misitu Tanzania (TFS) kutengeneza madawati 20,000 kwa nchi nzima na kuwataka maliasili kuyakamilisha kwa muda uliopangwa.

ìNinachotaka ni kukamilika kwa asilimia 39 ya madawati yaliobaki kwani hapa mmekamilisha asilimia 61 ya madawati 2,530, ili kwenda sawa na matakwa ya serikali lazima tufanye kazi kwa umakini na kufuata Ilani ya Chama kama Rais wa Jamhuri alivyoona changamoto katika sekta ya elimu na kuagiza kila mkoa kutengeneza madawatiî alisema Makani.

Alielekeza madawati hayo kupelekwa katika mikoa mitano ambayo yatagawiwa katika shule zilizo na upungufu wa madawati na kusema kuwa mengine yanatengenezwa katika mikoa tofauti, hivyo Mwanza kubaki na madawati 500, Kagera 700, Mara 450, Geita 450 na mkoa wa Simiyu madawati 430.

Injinia Makani alieleza kuwa TFS wamewaza kusaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa mbao za kutengeneza madawati hayo, huku kukiwa na changamoto ya ukataji wa miti pasipo kufuata taratibu na kukwamisha utengenezaji wa madawati kwa muda muafaka.

Aliwataka watu kutokata miti katika misitu ya asili bali wapande miti kwa wingi ili waweze kupata miti kwa shughuli za maendeleo, hasa katika hatua hiyo ya utengenezaji wa madawati baadaye.

ìJukumu la kulinda rasirimali ni la kwetu sote hivyo tujikumbushe kupanda miti kwa wingi na tukomeshe wale wote ambao wapo kwa ajili ya kuharibu rasirimali za nchi yetu,î alisema naibu waziri huyo.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa TFS, Dossantos Silayo alisema kumekuwa na changamoto ya baadhi ya watu kutumia agizo hilo vibaya kwa kujihusisha na vitendo vya uvunaji holela wa miti bila kuzingatia taratibu.

Silayo alisema kuwa wakala hautasita kuchukua hatua kwa vitendo vyovyote vya uvunaji, usafirishaji na biashara ya mbao itakayokiuka taratibu kwa visingizio vya madawati, kwani kila wilaya ina meneja na ofisa misitu hivyo amewataka wafuate taratibu za kupata malighafi hiyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.