Aliyetupa kichanga asakwa

MZALENDO - - HABARI - NA AHMED MAKONGO, BUNDA

JESHI la Polisi linamsaka mwanamke aliyejifungua mtoto kisha kumuweka ndani ya boksi na kumtupa katika Wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Limesema kuwa mtoto huyo alitupwa karibu na ofisi ya Wilaya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Bunda, ambapo mwili wa kichanga hicho cha jinsia ya kiume uligunduliwa na wananchi juzi jioni, ukiwa umetupwa katika mtaa wa Saranga.

Mashuhuda wa tukio hilo akiwemo katibu wa kitongoji cha Saranga Rubeni Zacharia, walilaani kitendo hicho cha ukatili na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha mwanamke aliyefanya unyama huo anakamatwa.

ìTunalaani kitendo hiki cha kinyama kilichofanywa na huyo mwanamke ambaye bado hatujamfahamu mtu anakubali kubeba mimba halafu anajifungua na kutupa kichanga hiki tena katika mazingira haya,î alisema Masalu Kiju.

Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ramadhani Ngíanzi, akizungumza kwa njia ya simu alithibitisha kuwepo tukio hilo na kusema kuwa upelelezi bado unaendelea.

Alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi kwa nia ya kumbaini aliyejifungua kichanga hicho, ili akamatwe na kufikishwa mahakamani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.