UWT yamlilia Mwenyekiti wake Dodoma

MZALENDO - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

UMOJA wa Wanawake Tanzania (UWT) umepokea kwa mshtuko na masikitiko taarifa za kifo cha Mwenyekiti wake mkoani Dodoma, Salome Kiwaya kilichotokea juzi kwa ajali ya gari.

Taarifa ya Katibu Mkuu wa UWT Taifa, Amina Makillagi, iliyotolewa jana ilisema Salome alifariki juzi kwa ajali ya gari iliyotokea mjini Dodoma.

Amina alisema UWT imempoteza kiongozi mahiri na makini ambaye enzi za uhai wake alikuwa mstari wa mbele kupigania Chama Cha Mapinduzi (CCM) na UWT.

Katibu Mkuu huyo alisema, familia imepata pigo kubwa kwa kumpoteza mpendwa wao, lakini UWT na wanachama kwa ujumla wana huzunika kwa kumpoteza kiongozi msikivu na mwenye uelewa wa hali ya juu.

Amina alisema mwili wa marehemu utaagwa leo mchana mjini Dodoma na kusafirishwa nyumbani kwao mkoani Njombe kwa mazishi.

Alisema UWT inatoa pole kwa ndugu, jamaa wana Dodoma, wanachama wote na wananchi kwa msiba huo mzito.

Amina aliwaomba wafiwa wote wawe na moyo wa uvumilivu katika kuomboleza msiba wa mpendwa wao.

Wakati huo huo, ratiba ya mazishi ya mwenyekiti huyo inaonyesha kuwa Salome ataagwa leo eneo la Imagi Kilimani kabla ya kusafirishwa kwenda Njombe kwa mazishi.

Salome alifariki juzi kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la Emausi, Kata ya Ipagala iliyohusisha magari matatu lori lenye namba za usajili T 716 CAY lililokuwa limepakia kichwa cha lo lenye namba za usajili T 152 BZN, Noa mali ya UWT mkoa ambalo namba zak hazikufahamika na Coaster ya Shule y Canon Andrea Mwaka.

Kwa mujibu wa ratiba, leo kuanzi saa mbili asubuhi mwili wa marehem utapelekwa nyumbani kwake ukitoke Hospitali ya Rufani ya Mkoa w Dodoma.

Baada ya hapo kutakuwa na salam mbalimbali za viongozi na makund maalumu kabla ya mwili huo kutolew na kupelekwa Kanisa Kuu la Roma Catholic.

Ratiba inaonyesha kuwa baada y misa, mwili wa marehemu utasafirishw kwenda Kijiji cha Mtila, Kata ya Matol mkoani Njombe kwa ajili ya mazik yanayotarajiwa kufanyika kesho.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.