Kipigo cha mwanafunzi Chinguku hakikubaliki

MZALENDO - - MAKALA -

Acha nikiri kwamba watoto wengi wa kizazi hiki cha karne ya 21 ya sayansi na teknolojia, wamekuwa wanaufahamu wa mambo mengi wakiwa katika umri mdogo, jambo linalochangia wajiamini na baadhi yao kuwa na viburi na dharau kwa watu walio wazidi umri.

Lakini kuna adhabu stahili ambazo wanafunzi watukutu kama inavyodaiwa ndivyo alivyokuwa Sebastian, ambazo zinalistahili kutolewa ikiwemo kupigwa viboko, lakini Msigwa na wenzake walimpiga isivyostahili.

Hata mwizi hastahili kupigwa bali anatakiwa kukamatwa, na kisha kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Jeshi la Polisi mara nyingi limekuwa likitoa rai au onyo kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi, sasa najiuliza ina maana Msigwa na wenzake walijiona wapo juu ya sheria kiasi cha kuamua kutoa aina ya adhabu ile?Hivi wangemuua Chinguku hata kama walikuwa sahihi wangejitetea kwa lipi hasa.

Nimpongeze Mkuu wa mkoa Mbeya, Makalla kwa hatua za haraka alizozichukua mara baada ya video hiyo kuanza kusambaa na ni miongoni mwa watu waliotumiwa na aliviagiza vyombo vya ulinzi na usalama, kulifanyia kazi suala hilo haraka iwezekanavyo na wampe taarifa.

Hapo ndipo utakapoona ya kwamba hii ni dunia ya utandawazi, dunia imekuwa sawa na kijiji kwani mitandao ya kijamii nayo imekuwa msaada mkubwa katika kufichua mambo mbalimbali ambayo awali ilikuwa ni vigumu.

Lakini ni hii mitandao ya kijamii, ambayo pia imekuwa mwiba mkubwa pale inapotumiwa tofauti na malengo yake, hatua ambayo inaweza kusababisha machafuko na mikwaruzano isiyo na msingi ndani ya jamii.

Umefika wakati sasa walimu wawe wanachekesha na kupima maneno ya kuyatumia mbele ya wanafunzi wao, hata kama wanakuwa na kosa, kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanawasaidia zaidi watoto kukua katika maadili na siyo kuwa chanzo cha mmomonyoko wa maadili.

Tukio la shule ya sekonmdari Mbeya , linatakiwa kuwa funzo kwa walimu kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamilifu, kwani walimu ni kundi muhimu katika ustawi na maendeleo ya nchi yoyote ile.

Hivyo baadhi ya walimu wanapokuwa na matendo na mambo ya ovyo, ni wazi hata wanafunzi watawaiga na mwisho wa siku tutakuwa na kizazi ambacho kitakuwa ni tatizo kwa ustawi wa taifa letu, katika kufikia maendeleo ya kweli.

Niwape hongera walimu ambao tangu waanze kazi hiyo wamekuwa wanasimamia miiko na misingi ya kazi hiyo, hatua inayowafanya waweze kuitendea haki taaluma hiyo muhimu kwa taifa lolote duniani.Msikubali baadhi ya walimu aina ya Msigwa wawachafulie sifa nzuri mbele ya jamii.

Huo NI MTAZAMO Suney27@yahoo.com au 0713-349299.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.