SUGLO Azaliwa viungo vya tumbo vikiwa nje

MZALENDO - - MBELE - ACCRA, Ghana

HUJAFA hujaumbika, ndivyo unaweza ukasema kutokana na mikasa ambayo binadamu amekuwa akikabiliana nayo kila kukicha.

Mikasa hiyo wakati mwingine huwafanya baadhi ya watu kukata tamaa ya kuishi kwa sababu ya kuamini kuwa, hawataweza kuondokana na maswahibu yanayowakabili.

Lakini hadithi ni tofauti kwa Ethan Suglo ambaye ana umri wa miaka mitatu alizaliwa sehemu kubwa ya viungo vyake vya tumboni vikiwa nje.

Viungo hivyo vilikuwa vilikuwa vikikua kadri umri wake ulivyozidi kusonga mbele, hivyo kuhatarisha usalama wa maisha yake.

Wazazi wake Suglo hawakuwa na fedha za kugharamia matibabu yake nje ya nchi na kipindi hicho chote walikuwa wakisubiri majaliwa ya Mungu katika kuokoa maisha yake.

Dk. David William ambaye ni raia wa Uingereza alikwenda nchini Ghana kumtembelea mtoto wake wa kike ambaye ni mwalimu wa Kiingereza na ni mtangazaji wa kituo kimoja cha redio.

Raia huyo wa Uingereza akiwa nchini humo alikutana na Charles Suglo ambaye alikuwa akifanya kazi ya utangazaji na na mtoto wake na ni baba mzazi wa Suglo.

Charled baada ya kukutana na daktari huyo alimweleza matatizo yanayomsumbua mtoto wake jambo lililosababisha ashindwe kumpeleka shule na kwamba kila anayemuona humshangaa na kumtolea maneno yasiyofaa.

Dk. William aliahidi kumsaidia mtoto huyo ili aweze kupata matibabu na kuwa katika hali ya kawaida kama binadamu wengine walivyo.

“Nilihitaji kuonana na mtoto huyo kwa sababu mimi ni daktari hivyo nafikiri anaweza kuwa na matatizo ya utapiamlo, lakini nilivyomuona nilishtuka.

“Sikuwahi kuiona hali hiyo. Sina uhakika kama nilishawahi kukutana na mgonjwa wa aina hiyo katika kipindi chote cha kazi. Nimefanya kazi ya udaktari kwa zaidi ya miaka 30 ..... sijawahi kuona ugonjwa huu,” anasema.

Baada ya kupewa habari ya kusikitisha kuhusu Ethan, Dk. Williams alihitaji kumfanyia uchunguzi wa kitaalamu mtoto huyo.

Dk. William alimweleza Charles kwamba atashirikiana na madaktari wengine kutoka Ghana au Nigeria kumfanyia upasuaji mtoto huyo.

Licha ya jitihada kubwa iliyofanywa na Dk. William, upasuaji huo ulishindikana kutokana na kutokuwepo kwa vifaa tiba na wataalamu wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo.

Kutokana na kazi kuwa ngumu, Dk. William alilazimika kuwasiliana na madaktari bingwa wa upasuaji nchini Uingereza, kwenye Hospitali ya John Radcliffe, ambao walisema wana uwezo wa kumfanyia Ethan, upasuaji.

Hata hivyo, madaktari hao walikumbana na kikwazo kikubwa katika kufanikisha uchunguzi huo kutokana na wazazi wake kutokuwa na fedha za kugharamia matibabu hayo nchini.

“Waliniambia itagharimu paundi 51,000 lakini fedha hizo ni vigumu kupatikana hivyo nilifanya hafla ya kukusanya fedha za kugharamia tiketi za ndege pamoja na gharama za matibabu,” anasema.

Julai, mwaka huu, baada ya kupatikana kwa fedha hizo Suglo alisafirishwa kwenda nchini Uingereza kwa ajili ya matibabu ili kuokoa maisha yake.

Hata hivyo, baada ya upasuaji kukamilika na kupata nafuu, Suglo amerejea juzi nchini Ghana na huwezi amini jinsi alivyokuwa na hali yake kwa sasa.

Suglo kwa sasa anacheza michezo mbalimbali na amekuwa mwenye furaha baada ya kupona tatizo lililokuiwa likimsumbua kwa muda.

SUGLO akiwa na baba yake mzazi, Charles Suglo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.