Makamu wa Rais awatoa hofu wafanyabiashara

MZALENDO - - MBELE - NA CHRISTOPHER LISSA NA SYLVIA SEBASTIAN

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kuboresha fursa na kuweka mazingira yenye tija kwa wafanyabishara,

Pia, amewatoa hofu kutotishwa na hali ilivyo hivi sasa ikiwa ni pamoja na kasi ya serikali katika ukusanyaji kodi.

Aidha, amesema kamwe serikali haitawavumilia wafanyabishara wa nje ambao hawafuati kanuni na taratibu wanazopewa wakiwa hapa nchini.

Makamu wa Rais aliyasema hayo jijini Dar es Salaam, jana, wakati akizindua rasmi Jumuia ya Wafanyabishara Wanawake Kariakoo (JUWABIKA).

Aliwataka wafanyabishara ambao walikimbia kupitisha mizigo yao katika Bandari ya Dar es Salaam, kurudi na kutoiogopa serikali kwenye kueleza matatizo yao.

“Hamuwezi kukimbia nyumbani, zungumzeni na serikali, acheni tabia za kuzungumza mambo pembeni,îalisema Samia.

Aliongeza kuwa wapo baadhi ya wafanyabiashara wanaojenga hofu hasa wakati huu serikali inapochukua hatua ikiwemo za kusimamia kikamilifu kodi na ushuru.

“Serikali inataka kujiendesha kwa kutumia mapato yake ya ndani , hivyo hali hii inapotokea ieleweke kuwa ni katika harakati za kujipanga si kuwabana nyie wafanyabishara. Tumeweza kununua ndege mbili kwa fedha zetu. Tunaendelea kuboresha miundombinu kwa fedha zetu wenyewe. Haya ni mafanikio makubwa katika kipindi kifupi,”alisema.

Kuhusu UWABIKA, Makamu wa Rais, aliwapongeza wanawake walioamua kwa dhati kuunda jumuia hiyo na kuwataka kuimarisha umoja huo na kuzingatia elimu ya bishara.

“Jambo muhimu si mtaji wala ofisi bali jambo la kwanza ni elimu ya jinsi ya kuendesha bishara,” alisema.

NAIBU Kiongozi wa Mkuu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia Ithnasheriya nchini, Sheikh Muhammad Abdi, akichangia damu, kuadhimisha kifo cha mjukuu wa Mtume Mohammad (SAW), Imam Hussein, Kigogo, Dar es Salaam. (Picha na Jumanne Gude).

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.