Rais Dk. Magufuli awakaribisha wafuasi wa Bohora kuwekeza

MZALENDO - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

RAIS Dk. John Magufuli, amewakaribisha wafuasi wa Madhehebu ya Bohora duniani kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali.

Wito huo aliutoa jana alipokuwa akihutubia tamasha la Madhehebu ya Bohora ambayo yalifanya maadhimisho ya dunia ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Kiislam jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho hayo yaliwaleta nchini wafuasi zaidi ya 30,000 kutoka nchi mbalimbali na kuongozwa na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani, Mtukufu Dk. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb (TUS).

Akihutubia wafuasi wa Bohora katika Msikiti wa Hakimi uliopo Upanga Jijini Dar es Salaam, Rais Dk, Magufuli alimshukuru Kiongozi Mkuu wa Bohora kwa kukubali kufanya maadhimisho ya mwaka mpya wa madhehebu hayo nchini.

Pia, aliwashukuru na kuwapongeza wafuasi wa madhehebu hayo kwa kukubali kuja nchini na kukaa kwa siku zote za maadhimisho hayo kuanzia Oktoba 2, walipoanza hadi Oktoba 11, mwaka huu watakapomaliza.

Rais Dk. Magufuli aliwapongeza viongozi na wafuasi wa Madhehebu ya Bohora kwa kutumia maadhimisho hayo kuhimiza amani, upendo na mshikamano.

Aidha, aliwashukuru kwa kushiriki katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ikiwemo mchango wa dola za Marekani 53,000 zilizotolewa na kiongozi mkuu wa Bohora kwa serikali kwa ajili ya kuchangia kampeni ya utengenezaji wa madawati na kuwaleta madaktari kutoka Hospitali ya Saifee ya India waliotoa matibabu bure kwa wananchi wa Arusha.

Hata hivyo, Rais Magufuli aliwakaribisha wafuasi wa Bohora duniani kuja kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, uvuvi, misitu, mifugo, madini na gesi.

Alisema kwa sasa soko la uhakika lipo ndani ya nchi, katika Jumuia ya Afrika Mashariki na Jumuia ya Maendeleo Kusin mwa Afrika (SADC) yenye wat takribani milioni 400.

Kwa upande wake, Kiongoz Mkuu wa Madhehebu ya Bohor Dk. Saheb (TUS), alimshukur Rais Dk. Magufuli kwa kuungan na wafuasi wa madhehebu y Bohora katika maadhimisho hayo

Alisema wafuasi wot wa Bohora wanahimizw kushirikiana na mamlaka zilizop katika nchi wanazoishi, kuwa rai wema na kufuata sheria.

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu, msaada wa dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya sh. milioni 30 vilivyotolewa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani humo, mjini Bukoba, jana. (Picha na Eleuteri Mangi wa MAELEZO).

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.